Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli Awaapisha Viongozi Saba (7) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Viongozi saba wakiwemo Mawaziri wawili, Naibu Mawaziri wanne, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mwita Waitara kuwa Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Joseph Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Constantine Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Japhet Ngailonga Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakishuhudia tukio hilo.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Innocent Bashugwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakishuhudia tukio hilo.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu January Msofe. kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria.
Viongozi mbalimbali waliopishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashugwa, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mwita Waitara pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msofe.
Viongozi mbalimbali waliopishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakisaini Hati za viapo vyao vya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Viongozi saba wakiwemo Mawaziri wawili, Naibu Mawaziri wanne, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msofe mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda pamoja na Waziri wa zamani wa Wizara hiyo Charles Mwijage mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakary Zebeiry mara baada ya hafla ya Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ngugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Kamishna wa Maadili Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela pamoja na Viongozi mbalimbali waliopishwa pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari waliofika Ikulu kwa ajili ya kutangaza tuko la Uapisho.
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.