Habari za Punde

Jumuiya ya Watanzania Ughaibuni Yapata Uongozi Mpya wa Mpito Huko Dallas,Texas, Marekani.


Wanajumuiya ya Watanzania Wanaoishi Ughaibuni  (Diaspora ) Nchini Marekani, Dallas,Texas .wakifuatilia Mkutano huo wa Uchaguzi wa Viongozi wa Mpito wakati wa mkutano huo, uliowachagua Viongozi wa Mpiti Mweweka Hazina, Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Muweka Hazina Bi Jocylne devosta.
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bw. Godfrey Mwamsoyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Everest Michael. 



Na.Buberwa Jackob


Kwa mujibu wa taarifa toka Jumuiya ijulikanayo kama Tanzanians Dallas, ambayo ni jamii ya watanzania wanaoishi katika jiji la Dallas, Texas na vitongoji vyake, limefanya mabadiliko siku ya Jumamosi tarehe 12, 2019 kwa kuwachagua viongozi mpito watatu. Uchaguzi huo ulihudhuliwa na wakazi wengi wa sehemu hizo zilizolizunguuka jiji la Dallas na kufanya maamuzi ya uongozi wa dharura kutokana na kujiudhuru kwa uongozi uliyopita.

Watanzania katika jiji hilo la Dallas na vitongoji vyake wanaamini kwamba, mshikamano wao ambao ndio kilikuwa ni chanzo kikubwa cha wao kuwa kitu kimoja wakati wa misiba na dharura za aina yote kimaishi wanavyoishi huko ughabuni. Kufuatana na katiba ya jumuiya hiyo hakuwa nabudi kuitisha kikao na kuwa na maamuzi ya kuteuwa wagombea mpito mpaka hapo mwezi Julai katika uchaguzi mkuu chini ya utaratibu  mpya.

Uongozi uliotumikia jumuiya hiyo kwa muda sasa na hatimae kujiudhuru kwa hiyari, ni mwenyekiti Bw. Benedict Kazora, Bi Maria Musomi, Makamo mwenyetkiti na Bi Viola  mbise, Katibu. Maamuzi hayo ya ghafla yaliwakilishwa kwenye kamati ya ushauri na kutangazwa rasmi katika tofuti za mitandao ya kijamii mara moja. Harakati zipo mbioni kuwasiliana na uongozi uliopita kukabidhiana nyaraka na uongozi mpya mpito haraka iwezekanovyo.

Jumuiya hiyo, imewachagua viongozi wake mpito wapya kupitia utaratibu wa kuwapigia kura wale wote walioteuliwa na wanajumuiya baada ya mkutano huo mahususi  kuziba hizo nafasi hizo. Yafuatayo ni majina ya wachaguliwa wapya,  Mwenyekiti ni Bw. Everest M. Michael, Katibu Bw. Godfrey Mwamsoyo na mweka hazina ni Bi Jocyline Vadesto. Wateuliwa wote hao ni wakazi wa Dallas na vitongoji vyake. Jumuiya mzima ya Watanzania Dallas inatoa pongezi na shukrani nyingi kwa wale wote walio pata wasaa na kujitokeza kufanya zoezi hili muhimu.

Pia vilevile, sambamba na mkutano huo lilichaguliwa baraza la ushuri la watu wa jumuiya hiyo  chini ya mapendekezo ya wanajumuiya wake, na sio tena kama jinsi baraza lile la zamani kuteuliwa na mwenyekiti. Hii ni kuhamasisha dhamira  na malengo  ya jamii kupewa kipaumbele katika maswala ya jamii hiyo. Misiba na matatizo yasiyo tabirika, ndivyo vigezo vikuu vilivyo waleta wanajumuiya hao pamoja na kusaidiana  kutatua yanayojiri wakati kama huo mgumu kwao.

Hivyo basi, baraza la ushauri lina takribani watu kumi na moja ambao watakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na uongozi wa juu na kujaribu kuwa na ufumbuzi wa matitizo au misiba inapotokea katika uzio wa mipaka ya vitongoji vyao. Hivyo,  walioteuliwa na jamii hiyo katika baraza au kamati hiyo hadi hapo mwezi Julai  uchaguzi mkuu ni:

1. Bw. AloyceChissanga.
2. Bw. Peter Kapanga. 
3.Bi Anna Ngoti. 
4.Bw. Felix Maganjila. 
5. Bw. Kibwana Rumadha.
6. Bi Arafa Manganji.
7. Bw. Ibrahim Kulindwa. 
8.Bi Rosemary Kessy.
9. Bw. Erick Joshua.
10. Bi Sofia Lesso.
11. Bw. Godlisten Lyimo.

Hao ndio wanaoiwakilisha baraza au kamati ya ushuri mpito iliyopo madarakani tokea uchaguzi wake wa tarehe 12 January mwaka 2019.
Juhudi zinaendelea kuhakikisha kwamba kwa mujibu wa katiba, yote yanayojiri katika makabidhiano ya kifedha na vitega uchumi ya Jumuiya vinatendwa chini ya utaratibu sahihi na wenye nidhamu. Hii utawapo urahisi fasaha wale viongozi wapya kufuatialia harakati zote zinazo husiana na jumuiya na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kupitia vivutio vyake asilia vya kitalii na maliasili.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa mwenyekiti mpya wa mpito, ndugu Everest,  inaeleza kwamba, kazi kubwa iliyopo ni kuwa hamasisha wanajumuiya wote wa asili ya Tanzania kushiriki katika ufumbuzi wa maswala yanayotukabiri na kuwa bora, imara zaidi ya jumuiya zinginezo toka Afrika. Tanzania, hususani sekta ya utalii, madini na nyanja nyinginezo  tofauti, tutazidi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha nchi yetu inazidi kutambulika hapa na kuwavutia jamaa na marafiki wetu wa Marekani  waje tembelea mbuga zetu za wanyama,  mlima wa Kilimanjaro na mengineyo zaidi toka Tanzania.

Mwisho kabisa, Jumuiya hiyo ya watanzania wanaoishi Dallas na vitongoji vyake vya karibu  pia  wakazi wake ambao kwa namna moja au nyingine waliowahi kuishi huko wanawatakia uongozi huu mafanikio mema yenye mshikamano wa dhati na  uzalando halisia kama Tanzania Diaspora.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.