Habari za Punde

MASAUNI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NJOMBE KUHUSU UTEKWAJI NA MAUAJI YA WATOTO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi  kuhusu matukio ya utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliwaasa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika juhudi za kukomesha matukio hayo
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri akizungumza na wananchi  kuhusu matukio ya utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliahidi kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kukomesha matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto
Mkazi wa Njombe, Alex Msupilo akimuuliza maswali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kukagua leseni za waganga wa tiba asilia ambao wamekua wakitajwa kufanya tiba chonganishi zinazopelekea kutokea kwa matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto katika mkoa huo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao kidogo kilichohusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe na baadhi ya wananchi lengo ikiwa ni kujadili juu ya matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.