Habari za Punde

Balozi Seif Azungumza Profesa Kabudi

Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipofika kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.







Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi alisema Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuwa na Taifa linaloendelea kudumu muda wote kutokana na misingi imara iliyowekwa na Waasisi wa Taifa hilo.
Alisema yapo Makabila mengi katika Mikoa na Wilaya mbali mbali Nchini Tanzania lakini muungano wa sauti moja inayozungumnzwa na Wananchi wake Bara na Zanzibar imekuwa mfano kwa Mataifa mengine Duniani.
Profesa Palamagamba Kabudi alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar alipofika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.
Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yaliyowahi kuunganisha Nchi zao akaitolea Mfano iliyokuwa Yugoslavia na sasa imesambaratika Senegal na Gambia kwa Afrika lakini zimeshindwa kuendeleza Miungano hiyo.
Waziri Palamagamba alisema wakati Serikali zote mbili Nchini Tanzania zinaendelea kuheshimu kwa kuweka Kumbukumbu za Waasisi hao Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Vizazi vya sasa vinapaswa kujifunza tabia ya Viongozi hao walioacha msingi imara wa Umoja ndani ya Ardhi ya Tanzania.
Akigusia suala la Diploma ya Uchumi ambayo kwa sasa Tanzania imeelezekeza nguvu zake kupitia Balozi zake zilizoko nje ya mipaka ya Nchi Profesa Palamagamba alisema Serikali inaendeleza mfumo wa kushawishi Wawekezaji ili kuunga mkono jitihada za Taifa za kuwa na Tanzania ya Viwanda ifikapo Mwaka 2025.
Alieleza kwamba jitihada zinafanywa za kutangaza uimarishaji wa fursa za Kiuchumi zinazopatikana kutokana na rasilami nyingi zilizopo Nchini ambazo uwekezaji wake unaweza kusaidia soko la ajira na mapato ya Taifa.
Alielezea umuhimu wa mkakati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Kuimarisha Uchumi wake unaopaswa kuendelea kuungwa mkono Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika muelekeo wa kuelekea kwenye Maendeleo ya haraka.
Akigusia Sekta ya Utalii inyoonekana Zanzibar kufanya vyema, Waziri Palamagamba alisema Sekta hii muhimu hivi sasa kwa mapato ya Taifa lazima iwekewe utaratibu wa pamoja utakaosaidia kuuza haiba ya pande zote mbili za Muungano.
Alisema vipo vivitio vinavyopaswa kutangazwa kwa pamoja Bara na Zanzibar ambavyo vinaweza kutoa nguvu ya ushawishi wa Watalii kufanya ziara ya makusudi ya kutembelea sehemu zote mbili kwa wakati mmoja.
Waziri huyo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielezea faraja yake kutokana na Zanzibar kupiga hata kubwa katika kuimarisha Sekta ya Utalii inayoonekana kutoa ajhira kubwa hasa kwa kundi kubwa la Vijana.
Alifahamisha kwamba ongezeko kubwa la idadi ya Watalii wanaotembelea Zanzibar inayopanda kila kukicha imethibitisha uwepo wa mafanikio katika kuendeleza Sekta hiyo muhimu.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ushawishi wa Uwekezaji ndani ya Visiwa vya Zanzibar unapaswa kuungwa mkono na Ofisi zote za Kibalozi za Tanzania zilizopo Mataifa mbali mbali Duniani.
Alisema Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ushawishi wake kwa Wawekezaji na Mataifa ya kigeni unawajibika kusimamiwa na Mabalozi wa Tanzania kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Balozi Seif alimueleza Profesa Palamagamba kwamba Zanzibar kupitia Viongozi wake wote waliopita na waliopo hivi sasa bado wanaendeleza sera na Mikakati iliyoacha na Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Alisema uimarishaji wa Miundombinu ya Mawasiliano, Ujenzi wa Nyumba za Kisasa za Maendeleo, Afya, Elimu pamoja na huduma za Maji safi na salama ni miongoni mwa Sekta zinazoendelea kuimarishwa na Viongozi wote.
Balozi Seif  Miradi iliyobuniwa na Serikali ya Mapinduzi ya ujenzi wa Miji Mipya kama ule wa Ng’ambo tuitakayo katika eneo la Kwahani na Mtaa wa Chumbuni imelenga kustawisha maisha ya Wananchi wake ili kuachana na matumizi mabaya ya Ardhi ndogo iliyopo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.