Habari za Punde

Maulamaa Watakiwa Kuwa na Hofu ya Allah Kwa Vile Wamebeba Dhima

Na.Raya Hamad .WKS.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi amelitaka Baraza la Maulamaa nchini kuwaelimisha Waumini wa Dini ya Kiislamu kuvumiliana katika tofauti   ndogo ndogo na kuzipatia ufumbuzi  ili amani na utulivu  iendelee kutawala nchini kwa kutatua migogoro katika misingi ya Dini ya Kiislamu.

Sheikh Kaabi ameyasema hayo katika kikao cha 3 Baraza la 5 la Maulamaa Zanzibar kwenye ukumbi wa Mkutano Mazizini ambako amewasisitiza   Maulamaa kuwa na khofu ya Allah kwa vile wanabeba dhima ya wanaowaongoza
"Macho imani za  ya waumini  wa Dini ya Kiislamu yanawatazameni nyie hivyo msiridhike na Elimu mliyonayo na ndio maana tunaambiwa tutafute Elimu mpaka uchina  ili mtakapotowa hukumu na khatwa  basi ziwe zinazoendana na misingi ya Dini yetu  na tuiogope kalamu ya  Allah "alisitiza

Aidha amewaomba Maulamaa hao kuhakikisha Maeneo wanayoyasimamia yako salama ikiwemo kuwaelewesha Maimamu namna ya kuepuka mizozo inayojitokeza ndani ya misikiti, kuwatahadharisha wageni wanaokuja kwa ajili ya kuja kutoa   daawa kufuata sheria za nchi  na sio kufarakanisha waumini kutokana  na madhehebu .  

Hivi karibuni kumezuka tabia kwa baadhi ya kikundi  kukashifu viongozi  wa Dini Masheikh na Maulamaa ambako wengine wamekwisha tangukia mbele ya hali   na kusema kuwa si sahihi na ni marufuku kufanya hivyo . 
 Baraza la Maulamaa kwa kauli moja limewaagiza walimu wa Madrasa zote nchini kutowachukuwa katika sherehe na shughuli za Maulid Watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wakati wa usiku kuanzia saa 2 jambo ambalo limeelezwa linachangia kwa kiasi kikubwa  udhalilishaji na ubakaji unaofanywa na baadhi ya walimu waliokosa uadilifu na utu  .

Baraza limefafanua kuwa     kesi nyingi  za ubakaji na udhalilishaji  zilizoripotiwa  na kushitakiwa ambazo zimetokana na  Madrasa chanzo chake ni sherehe za usiku hivyo  kwa agizo hili  Watoto walio chini ya  umri wa miaka 18 shughuli watazopaswa kushiriki ni zile za asubuhi mpaka saa moja usiku.

Aidha  Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Soraga  amewaomba Masheikh kujitahidi kuwaelimisha waumini kwa njia tofauti ikiwemo kutumia  khutba msikitini   Vyombo vya habari, Darsa, Baraza za mazungumzo  ili jamii iendelee kushikamana  na Dini na kupata ufumbuzi wa baadhi ya masuala ambayo yanajibika na kutatuka bila ya kufikishana kwenye vyombo vya sheria kwa vile  Baraza lina uwezo na kisheria  wa kutatua migogoro na kuchukuwa uwamuzi unaofaa .

Kikao cha Maulamaa kimehudhuriwa  na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis, Naibu Kadhi Sheikh   Hassan Othman 
Ngwali, Naibu Mufti Sheikh Mahmoud Wadi  pamoja na Wajumbe wengine. 

Kifungu cha  15 cha sheria ya Mufti nimempa Mamlaka Waziri husika kutunga kanuni ambapo miongoni mwa kanuni ni kuwepo kwa Kanuni ya Baraza la Maulamaa ya 2002.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.