Habari za Punde

Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar Wajumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar Katika Futari Aliyowaandalia Katika Makazi Yao Mazizini Zanzibar.


Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico, akizungumza na kutowa neno la shukrani kwa Niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, baada ya kumalizika kwa futari maalum aliyowaandalia Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Maziziniu Zanzibar. 

WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Moudline Castico ameipongeza jamii ya Wazanzibar kwa juhudi inazozichukuwa katika utunzaji wa familia, na hivyo kupunguza tatizo la utupaji wa watoto ovyo.

Ametowa pongezi hizo  kituo cha kulelea watoto Mazizini, wakati akitowa neno la shukrani baada ya hafla ya Futari iliyoandaliwa kwa  pamoja kati ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Suleiman Idd, kwa ajili ya watoto wa kituo hicho.

Alisema ni jambo la faraja kuona katika siku za hivi karibuni vitendo ya utupaji wa watoto vimepungua, hatua aliyobainisha inatokana na juhudi za wananchi katika utunzaji wa familia zao.

Aliiomba jamii kuendelea na juhudi hizo zinazotokana na ushirikiano wa pamoja kati ya jamii hiyo na Serikali.

Aidha, Waziri Castico alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi hao kutokana na mchango mkubwa wanaouonyeha katika kuleta maendeleo na ustawi bora wa watoto hapa nchini, ikiwemo wale wanaoishi katika mazingira magumu.

Alisema hafla hiyo iliyowahusisha watoto wanaolelewa katika kijiji hicho inadhihirisha imani na mapenzi makubwa waliyonayo viongozi hao kwa watoto hao, hivyo akawaomba kuendelea kuwa karibu nao katika vipindi vyote.

Katika hatua nyengine, Waziri Castico aliutaka uongozi wa kituo hicho kuendelea kuwatunza vyema watoto hao, sambamba na kutoa indhari ya  kuwepo umakini wa kiusalama katika kipindi cha sherehe ya sikukuu ya Idd el Fitri.

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 
 E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.