Habari za Punde

Balozi Seif akutana na Uongozi wa Benki ya Africa (BOA)

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Uongozi wa Benki ya Afrika Tawi la Zanzibar  chini ya Memeja wake Nd. Juma Burhan Mohamed aliyepo kati kati
 Meneja wa Benki ya Afrika Tawi la Zanzibar Nd. Juma Burhan Mohamed kati kati akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa pili kutoka Kulia.
 Balozi Seif Kulia akijaza fomu za kufungua Akaunti ya kujiunga rasmi na Benki ya Afrika {BOA} hapo katika Majengo ya Baraza la Wawakilishi Chukwani.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizishauri Taasisi za Kibenki kutoa mikopo nafuu itakayokuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya Wananchi.
Meneja wa Benki ya Afrika Tawi la Zanzibar Nd. Juma Burhan Mohamed akisisitiza akifafanua baadhi ya mikopo inayotolewa na Benki yake iliyoanzishwa Tawi lake Zanzibar karibu Miaka Mitatu sasa.

Na Othman Khamis/ Rashida Abdi OMPR

Uongozi wa Benki ya Afrika {BOA} Umeshaamua kushirikiana na Serikali Kuu wakati wowote katika mueleko wa unazishwaji wa Miradi ya Kiuchumi na Maendeleo itakayoleta tija ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Taifa na kuimarisha Ustawi wa Wananchi.
Meneja wa Benki ya Afrika Tawi la Zanzibar Nd. Juma Burhan Mohamed alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyeamua kufungua Akaunti ya Benki hiyo tukio lililofanyika katika Ofisi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi iliyopo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Meneja Juma Burhan alisema Benki hiyo tayari imeshajipanga kutekeleza Mpango huo utakaoridhiwa kwa kutoa Mikopo kwenye Miradi mikubwa na midogo itakayoanzishwa Nchini ikiwemo ile inayobuniwa na Wananchi wa kipato cha chini katika makundi ya Ushirika pamoja na Saccos.
Alisema hivi sasa Taasisi hiyo ya Fedha iliyopata mafanikio makubwa ndani ya kipindi cha Miaka Mitatu tokea kuanzishwa kwake Zanzibar imeanza na harakati za kutoa Mikopo kwa Watendaji waliomo ndani ya Wizara ya Kilimo kwa utaratibu wa kukopeshwa mteja hadi asilimia 60%.
Nd. Burhan alifahamisha kwamba mikopo hiyo ina nia ya kuwainua kiustawi Wafanyakazi wa Taasisi za Umma katika kuwezeshwa kuchukuwa mikopo itakayowapa fursa za kupata Nyumba, Gari kujisomesha mwenyewe na hata kusomesha Mtoto wake.
“ Tumejipanga kuendelea kutoa huduma zitakazokidhi kiu na mahitaji ya Wananchi licha ya kuelewa kwamba Biashara ya Benki sio rahisi kwa vile inahitaji umahiri na umakini ambao unapatikana ndani ya Taasisi yao”. Alisema Nd. Juma Burhan.
Meneja huyo wa Benki ya Afrika Tawi la Zanzibar alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba mpango huo unalenga kumjengea mazingira bora ya Ustawi Mwananchi tokea udogo wake, pale anapopata ajira hadi kustaafu kwake kutakakomuwezesha kukopa ili mafao yake yaendelee kubakia hakiba katika maisha yake ya uzeeni.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliushauri Uongozi wa Taasisi za Kibenki kuendelea kutoa mikopo itakayokuwa nafuu  kwa vile Wananchi walio wengi uwezo wao bado mdogo.
Balozi Seif alisema Wananchi mbali mbali wakiwemo Watumishi wa Umma na wale wa Vijijini na Mitaani wanahitaji nguvu za uwezeshaji katika kujiendesha kiuchumi ili wapambane na ukali za Maisha.
Alisema Zanzibar kwa kuwa inazalisha zaidi ya Wasomi 3,000 kila Mwaka Serikali inaendelea kushajiisha Wananchi ili waweze kuwa na fursa za kujiajiri wenyewe mpango ambao tayari umeshaanza kuungwa mkono na Jamii na hasa kwa Vijana na Wanawake.
Balozi Seif alisisitiza kwamba Elimu ya Wasomi hao kwa sasa ni vyema ikaelekezwa katika fani ya ujasiri Amali itakayowezesha kutoa soko la ajira katika Taasisi za Umma na zaidi zile Binafsi Mitaani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi huo wa Benki ya Afrika kwamba Serikali Kuu itatoa kila aina ya msaada unaohitajika katika kuona malengo au majukumu ya Benki hiyo yanafanikiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.