Habari za Punde

Timu zinazoshiriki Kipwida Cup zalalamika waamuzi kutotenda haki

NA MWAJUMA JUMA


BAADHI ya viongozi wa timu zinazoshiriki ligi ya Kipwida zimeanza kutoa malalamiko yao kwa waamuzi kwa kudai kutotendewa haki wakati wanapocheza.

Lalalmiko hilo limetolewa na kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Njaa Kali Issa Mohammed  Abdalla alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya mchezo kati yake na timu ya Mazombi ambao
ulimalizika kwa sare ya kutokufungana.

Alisema kuwa waamuzi kweli ni binadamu kuna mambo yanatokea yanakuwa nje ya uwezo wao lakini baadhi ya mambo yanatokea wanayaaachia kwa makusudi.

“Ni matatizo ya Kibinadamu lakini ni changamoto kwa upande wa mpira wa miguu ni lazima wawe makini wanapochezesha”, alisema.

Alisema kuwa anashukuru timu zote zimecheza vizuri na zilijitahidi kulenga mashambulizi lakini washambuliaji wake hawakuwa na bahati kwao na badala yake kumaliza wakiwa na sare hiyo.

Hata hivyo alisema kuwa katika mechi zijazo wanajipanga ili kuhakikisha wanafanya vizuri  ili kuwaridhisha mashabiki wao.

“Hatukuwa na bahati ya kuweza kushinda kwani tulijipanga vizuri na tunatarajia mchezo ujao tutafanya vizuri”, alisema.

Hivyo aliwataka mashabiki wao kutovunjika moyo na matokeo ya mchezo huo na kwamba uongozi wao benchi la ufundi unajipanga kuhakikisha mechi zinazofata wanafanya vizuri.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.