Habari za Punde

Balozi Seif Akabidhi Vifaa Vya Michezo Jimbo la Mahonda

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibat na Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Mbunge wa Jimbo hilo  Bahati Abeid Nassir wakizungumza na Wanamichezo wa Mpiura wa Pete wa Timu za Wadi za Mahonda na Fujoni kabla ya kuwakabidhi vifaa vya Michezo hapo Tawi la CCM Kitope “B”. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  na Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Zanzibar.Mhe. Balozi Seif na Mbunge Bahati wakiwakabidhi Vifaa vya Michezo Viongozi wa Timu ya Mpira wa Pete ya Fujoni Mwanafatu Othman na Ramla Said.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  na Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Zanzibar.Mhe.Balozi Seif na Mbunge Bahati wakiwakabidhi Vifaa vya Michezo Viongozi wa Timu ya Mpira wa Pete ya Mahonda Zawadi Aley na Zainab Issa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  na Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Zanzibar.Mhe.Balozi Seif akimkabidhi Kepteni wa Timu ya Mpira wa Pete ya Mahonda Fedha za Usafiri wa wachezaji hao kwa ajili ya kushiriki mchezo wa majaribio huko Mkokotoni Mkoa Kaskazini Unaguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Azma ya Uongozi wa Jimbo la Mahonda bado ipo pale pale katika kuhakikisha inaimarisha Micheo ili ifikie siku Jimbo hilo liwe na Timu iliyopevuka kimichezo na kushiriki Mashindano makubwa zaidi ya Kimataifa.
Mwakilidhi wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla fupi ya kuzikabidhi Vifaa vya Michezo Timu mbili za Mpira wa Pete {Netball} za Wadi za Mahonda na Fujoni iliyofanyika katika Ukumbi wa Tawi la CCM Kitope “B” Wilaya ya Kaskazini B.
Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi Vifaa hivyo kukamilisha ahadi iliyotolewa na Mke wake Mama Asha Suleiman Iddi aliyoitoa baada ya kushuhudia pambano la kirafiki la Mchezo wa Mpira wa Pete {Netball} uliozikutanisha Timu za Madada wa Fujoni dhidi ya Kitope lililofanyika katika uwanja wa mahonda Kiwandani mnamo Tarehe 5 Febuari Mwaka huu wa 2019.
Alisema uimarishaji huo wa Michezo ndani ya Jimbo hilo unakwenda sambamba na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuimarisha Sekta ya Michezo wa vile hivi sasa mbali ya kusaidia kulinda afya lakini pia imekuwa soko la ajira.
Balozi Seif aliwaomba Vijana wa Kike mbali ya kuendeleza mchezo wa Pete lakini pia wana fursa ya kuandaa Timu ya Jimbo ya mpira wa soka kwa vile tayari upo muelekeo wa kuimarika kwa mchezo huo kwa upande wa akina mama kama hivi sasa inavyoonekana kwenye mashindano ya Dunia ya Soka la Wanawake.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mahonda Bahati Abeid Nassir amesema inapendeza kuona hivi sasa vijana wengi wa kike wamehamasika kushiriki kwenye michezo mbali mbali inayoongeza ajira hasa Vikosini.
Mbunge Bahati aliwataka Wanawake hao wa timu za Mpira wa Pete wa Wadi za Mahonda na Fujoni wafanye mazoezi kwa malengo na kuacha ile tabia ya kuonekana Baadhi ya Wanawake hao huharibika kwenye Michezo jambo ambalo halipendezi hata kidogo.
Aliwaahidi Vijana hao wa kike kwamba iwapo watashinda kwenye mashindano yanayowakabili atakuwa tayari kuwaandalia safari ya matembezi ili kubadilisha mawazo kwa vile kutembea ni kusoma.
Katika hafla hiyo Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi Seti mbili za Jezi zilizokamilika Mipira, Viatu pamoja na Fedha za Soksi kwa Timu hizo za Mpira wa Pete za Wadi ya Mahonda na Fujoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.