Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akifafanua Jambo kuhusu Mkutano wa Wakuu
wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, alipokuwa katika
mahojiano ya kipindi cha 360 katika kituo cha Televisheni (Clouds TV)
yaliyofanyika leo Agosti 14, 2019 katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julias Nyerere Jijini Dar es Salaa, kulia ni
Mtangazaji wa Kipindi hicho, Baby Kabaye.
Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO 14.08.2019
Nchi 16 za Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimethibitisha kushiri Mkutano wa 39 wa
Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika
Jijini Dar es Salaam, Tanzania
Agost 17 na 18 mwaka huu.
Akizungumza katika
Kipindi cha 360 cha Clouds Tv, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi alisema maandalizi yamekalika na sasa
Tanzania iko tayari kwa ugeni huo.
Dkt. Abbasi alisema kuwa
mkutano huo ulitanguliwa na matukio mbalimbali ikiwemo Maonesho ya Wiki ya Viwanda
kutoka nchi wanachama wa SADC, Vikao vya Maafisa Waandamizi kutoka SADC, Vikao
vya Mawaziri kutoka SADC na Mikutano mbalimbali ya sekta za SADC, ambapo maeneo
haya yote Tanzania inachukua uenyekiti wa Nchi Wanachama.
“ Katika mikutano yote
iliyotangulia karibu nafasi zote za SADC kuanzia zile za kusimamia kamati,
kusimamia mabaraza mbalimbali, Tanzania imechukua hatamu, kwani kuna sekta
nyingi sasa zimeshachukua uenyekiti, Juzi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri
wa Anga Tanzania alichukua kiti hicho
cha kwenye kamati ya wanachama wa SADC, vilevile
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania naye alichukua nafasi hiyo
kwenye Kamati ya Mawasiliano SADC”, Dkt. Hassan Abbasi.
Dkt.Abbasi alisema kuwa
kuelekea kwenye tukio lenyewe ambalo ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Wafalme
kutoka Serikali 16 za nchi wanachama, zimethibitisha kushiriki mkutano huo na
kuwa viongozi wao wataanza kufika nchini kuanzia tarehe 15 na kuendelea.
Aidha Dkt.Abbasi alisema
kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa Kitovu cha Amani kwa nchi za kusini mwa Afrika, kwa
hiyo viongozi wengi wa nchi hizo watakuja Tanzania kama wanarudi nyumbani,
ambako ni kituo cha ukombozi wa nchi zao, na kufanya mkutano ambapo Agost 17 na
18 Wakuu wa Nchi Wanachama watasaini
mikataba mbalimbali na kuhitimisha ajenda zao.
Aliongeza kuwa kabla ya
kufika mkutano wa wakuu wa nchi kuna matukio mengine kama vile Mabalozi na
wawakilishi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali kuwasili nchini; ikiwa ni lengo
la kushiriki Mkutano Mkuu ambapo pia wamepata wasaa wa kufanya ziara katika
miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
“Kabla ya kufika Mkutano
Mkuu, kuna matukio mbalimbali ambayo pia ni makubwa na ni muhimu sana kwa nchi
yetu, leo tunatukio kubwa la Mabalozi 42 wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali
duniani wanatembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project( JK HPP) na kesho
watatembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) na hawa wote wako nchini
kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkuu wa SADC”, Alisisitiza Dkt.Abbasi.
Dkt.Abbasi alisema kuwa
Mabalozi hao wamekwenda kuona kwa mfano, ni nini serikali yao inatekeleza ili
wakirudi katika maeneo yao ya kazi wapate kuyatangaza waliyoyaona na kuweza
kuleta wawekezaji watakao kuja kuwekeza nchini na kuleta mapato kwa taifa.
Pia, Dkt. Abbasi alisema
kuwa leo Tanzania itampokea Rais wa
Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ambaye atawasili nchini kwa ziara ya siku mbili
kabla ya Kusiriki Mkutano Mkuu, na ziara yake itajikita zaidi katika kutembelea
eneo la wapigania uhuru Mazimbu, Mkoani Morogoro, ili kujenga kumbukizi ya
Udungu kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi,
akifafanua Jambo kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Nchi za Kusini
mwa Afrika SADC, alipokuwa katika mahojiano ya kipindi cha 360 katika kituo cha
Televisheni (Clouds TV) yaliyofanyika leo Agosti 14, 2019 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
Julias Nyerere Jijini Dar es Salaa, kulia ni Mtangazaji wa Kipindi hicho, Baby
Kabaye.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akieleza Jambo kuhusu Mkutano wa Wakuu wa
Nchi za Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, alipokuwa katika mahojiano
ya kipindi cha 360 katika kituo cha Televisheni
(Clouds TV) yaliyofanyika leo Agosti 14, 2019
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julias Nyerere Jijini Dar es
Salaa, kulia ni Mtangazaji wa Kipindi hicho, Baby Kabaye.
(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment