Habari za Punde

Maadhimisho ya siku ya Maafa Duniani yafanyika Zanzibar

 Baadhi ya Wageni Waalikwa waliohudhuria katika Maadhimisho ya siku ya Maafa Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil kikwajuni Zanzibar.
 Muasilishaji mada kutoka mradi wa Uimarishaji mji wa Zanzibar (ZUSP)Makame Ali Makame akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya Mradi katika  Maadhimisho ya siku ya Maafa Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil kikwajuni Zanzibar.
 Mkurugenzi mtendaji Kamisheni ya Maafa Makame Khatib akitoa maelezo kuhusu kamisheni katika  Maadhimisho ya siku ya Maafa Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil kikwajuni Zanzibar. 
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Abdalla Mitawi akizungumza machache kuhusu namna ya kudhibiti maafa katika  Maadhimisho ya siku ya Maafa Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil kikwajuni Zanzibar. 

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mihayo Juma Nhunga akitoa maelezo kuhusu maafa na kumkaribisha mgeni rasmi katika  Maadhimisho ya siku ya Maafa Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil kikwajuni Zanzibar. 



Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dk,Sira Ubwa Mamboya akitoa hotuba katika  Maadhimisho ya siku ya Maafa Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar. 

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR

Na Khadija Khamis –Maelezo- Zanzibar                  .
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirisha Dkt Sira Ubwa Mamboya ameitaka jamii kuchukua hatua za kujikinga na kujilinda katika uchafuzi wa mazingira ili kukabiliana na maafa.
Alisema kufanya hivyo kutasaidia kujiepusha na majanga mbali mbali ikiwemo maradhi ya mripuko  pamoja na mafuriko katika sehemu mbali mbali za miji na vijiji.
Hayo  aliyasema huko katika ukumbi wa Shekhe Idrisa Abdulwakili, Kikwajuni wakati wa Maadhmisho ya Siku ya Maafa Duniani yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais.
Alisema kuwa jamii iko haja ya kuzingatia  matumizi sahihi ya baharini na nchi kavu ili kuepukana na uharibifu wa mazingira unaotokana na binaadamu ambao husababisha majanga na adhari ya maisha ya watu .
Aidha aliwataka masheha kusimamia maeneo yao ili kulinda miundombinu zisiweze kuharibiwa jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya taifa .
Alisema serikali inaendelea na juhudi za kuwahakikishia wananchi wanaishi katika hali ya usalama kwa kutatua changamoto zilizopo kwa kuimarisha miundombinu za kisasa ikiwemo barabara na mitaro ya maji ya mvua.
Nae Naibu Waziri  Ofisi ya Makamo Pili wa Rais Mihayo Juma N’hunga alizitaka mamlaka za Serikali za mitaa kuimarisha usafi hasa katika kipindi hichi cha mvua za vuli ili kutekeleza vyema sheria namba 1 ya mwaka 2015 ya kukabiliana na maafa .
Aliwashukuru sekta binafsi ambazo zinaonyesha juhudi kubwa ya kufanya kazi kwa  mashirikiana na kamisheni ya kuakabiliana na maafa kwa kuondoa na kujitayarisha kwa aina yoyote ya majanga ambayo yanaweza kutokea
Naibu huyo alisema Serikali imeweza kujenga Miundombinu imara katika meaneo ya bahari, Vituo vya uokozi ,kitengo maalumu cha dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja,  kununua magari ya zimamoto na mambo mengine mengi ili kuimarisha usalama wa wananchi wake .
Kwa upande wa Afisa wa Kamisheni ya Maafa Makame Ame Simai alifahamisha aina za mjanga ambayo husababishwa na binaadamu na yanayotokana na tabia ya nchi ikiwemo kimbunga upepo mkali mafuriko, wadudu wa mimea, moto, kuharibika kwa huduma muhimu za jamii ikiwemo miundombinu ya barabara, na mengineyo ambayo  huleta adhari katika nchi
Alisema majanga yanayoadhiri mara kwa mara hapa Zanzibar ni mafuriko ambayo  nyumba nyingi huingia maji na hupelekea mripuko ya maradhi ikiwemo kipindupindu .
Nae Makame Ali Makame alisema Serikali imekusudia kuondoa maji ya mvua katika sehemu zote hatarishi na hadi sasa tayari imekwisha kufanikiwa kuondoa maji ya mvua yanayotuwama katika maeneo ya  Mnazimmoja, Kijangwani, Kariakoo Kwamtumwajeni, Magomeni Kwa bitihamrani Jan’gombe, Mtopepo, Kwamzushi hadi Karakana.
Hata hivyo alisema ujenzi wa mtaro wa kuondoa maji kutoka Mwanakwerekwe Kwamtumwajeni Viwanda vidogovidogo. Sebleni Lumumba hadi baharini bado unaendelea kujengwa chini ya usimamizi  wa ZUPC.
Aliwataka wananchi kuchukua hatua binafsi za kuzithamini juhudi za Serikali ili  kuzienzi kuzitunza miundombinu zinazojengwa ili kufikia lengo lililokusudiwa,la kuwapatia maisha bora wananchi wa Zanzibar .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.