Imeandikwa na Mwandishi wetu – Pemba
Wanafunzi wasiopungua 25 wa skuli ya msingi na chekechea ya Ziwani Mkoa wa Kaskazini Pemba wanadaiwa kudhalilishana kwa kulawitiana na kubakana baina yao hali ambayo imeleta mshituko kwa walimu hata kamati ya skuli hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo Bi Salma Ali Muhidin amesema chanzo cha kujua taarifa hizo ni baada ya kuwaona watoto hao hawapo sawa , wengine wakionekana kutokua na furaha, wengine wamekua na harakati nyingi na mabadiliko mengine, ambapo ndipo kulipopelekea kuanza mchakato wa kuwahoji ili kujua tatizo.
Akiendelea kueleza mwalimu huyo alisema, baada ya kuwahoji ndipo ilipofichukua siri ya kuwa , wanamchezo wa kudhalilishana wenyewe kwa wenyewe
“wengine walisema, wanapakatana, wanatiana vidole, na wengine ndio hivyo mpaka hayo washafanyiana” alisema mwalimu huyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa skuli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Mkubwa Abdulla Bakari alisema, katika harakati zake za kila siku, siku hiyo alibahatika kupita skuli na akawaona walimu wakiwahoji watoto juu ya tukio hilo.
Alisema, siku ya pili taarifa hizo zilienea zaidi na ikaamulika watoto hao waitwe kuhojiwa mmoja baada ya mwengine na kila mmoja akasema alivyofanyiwa
“wahusika wa kuu ni watoto wakubwa sio hawa, watoto chekechekea wahayajui kabisa matendo haya, sasa hivi tunataka tuwafanyie utafiti hawa wakubwa ili tuwapate, huu ni moto na unavongonya ndani kwa ndani” alisema mwenyekiti huyo.
Bi Asha Abdi kutoka chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA upande wa Zanzibar ambao ni wadau wakubwa wa kusaidia kuondosha vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto nchini alisema, wamezipokea taarifa hizo kwa huzuni kubwa huku akiashiria kuwa kuna haja ya kuchukuliwa hatua za ziada ikiwamo kuwezeshwa watoto wenyewe kujitambua pamoja na kuwezeshwa wazazi kujenga utaratibu wa kuwafuatilia watoto wao.
“walimu pia wawafuatilia kwa umakini sana wanafunzi wao”
Watoto hao ni mchanganyiko wa kike na kiume na wote hakuna aliyefikia umri wa miaka 18.
No comments:
Post a Comment