Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi
(katikati), akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile (kushoto) na Naibu Katibu
Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Ally Possi, mara
baada ya kuwasili katika Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani
iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala
mwaka wa Tatu, Rose Mweleka, akiwasilisha mada kuhusu jinsi ya kutekeleza haki
za watoto wa kike ikiwemo kuwafundisha hatua za makuzi ili kuwawezesha
kukabiliana na hali wakifikia umri husika, Mada hiyo iliwasilishwa kwenye
Maadhimisho ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi
(kulia), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile, baada ya kuwasili katika Sherehe za
Kuadhimisha ya Siku ya Haki ya Mtoto Duniani iliyofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, leo Novemba 20, 2019, ambako alialikwa
kuwa mgeni Rasmi.
No comments:
Post a Comment