Habari za Punde

Maadhimisho ya miaka 56 ya Zanzibar yalivyofanyika Uwanja wa Amaan

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume, Mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, alipowasili katika jukwaa kuu, wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania. Mhe. Benjaman Mkapa, alipowasili katika jukwaa kuu kuhudhuria hafla ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, alipowasili katika jukwaa kuu wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wac Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, alipowasili katika jukwaa la Viongozi kuhudhuria hafla ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar,( kulia kwa Dkt.Kikwete) Rais Mstaaf wa Zanzibar. Mhe.Dkt. Amani Karume.
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe.Dkt. Amani Karume na (katikati ) Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete.
 KIKOSI cha Bendera kikipita kwa mwendo wa pole pole wakitowa salamu za heshima wakati wa gwaride rasmin la kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
 GWARIDE la Kikosi cha JWTZ wakipita kwa mwendo wa pole pole mbele ya mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) wakati likipita katika jukwaa kuu la Viongozi  Uwanja wa Amaan Zanzibar.
 GWAride la Kikosi cha JWTZ Wanawake wakitowa heshima kwa mgeni Rais Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) wakipita kwa mwendo wa pole wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar,hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
 GWARIDE la Kikosi cha FFU wakipita kwa mwendo wa polepole wakati wa maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
 GWARIDE la Kikosi cha Jeshi pa Polisi Wanawake wakipita kwa mwendo wa kasi wakati wa hafla ya maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.

 GWARIDE la Kikosi cha KMKM Wanaume wakipita kwa mwendo wa kasi wakati wa hafla ya maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
KIKOSI cha Makomando wa JWTZ wakipita kwa ukakamavu wakati wa Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Amaan.
ASKARI wa zamani wa Tarabushi wakionesha umahiri wa gwaride la Mkoloni wakati wa Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilozofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.