Na Mwashungi Tahir Maelezo.
Waziri wa Kazi , Uwezeshaji ,Wazee, Wanawake na Watoto Moudline Cyrus Castico amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na chuo cha mafunzo kwa kuweka mazingira mazuri katika ujenzi wa kukerebisha tabia kwa watoto
Amesema ujenzi wa jengo la kurekebisha watoto kutapelekea kurahisisha utekelezaji wa sheria ya mtoto na 6 ya mwaka 2011 ya Zanzibar inayo wataka watoto kujengewa mazingira rafiki ili kuimarisha ustawi wao.
Akizungumza kwa niaba yake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Shadya Mohamed Suleiman wakati alipokua katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa Chuo cha kurekebisha watoto huko Hanyegwa Mchana ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Amesema kuwepo kwa changamoto ya mlimbukano wa watoto wengi wanao letwa katika vyuo vya mafunzo kumepelekea Serikali kujenga jengo hilo ambalo litasadia kuwaekea mazingira mazuri watoto hao katika kipindi chote cha mafunzo ya kurekebisha tabia .
Aidha alisema hakuna jambo zuri kama kumpa mtoto malezi bora mapema samaki mkunje bado mbichi kwani watoto watapofundishwa maadili mazuri mapema kutasaidia makuzi yao kupatikana Taifa lililo bora.
“hakuna jambo zuri kama kumkerebisha mtoto mapema kwani samaki angali mbichi akiwa mkavu hakunjiki bali anavunjika “ , alisema Naibu Waziri huyo.
Aidha amesema Serikali ya M apinduzi ya Zanzibar imeona kuwepo kwa chuo cha mafunzo cha la kurekebish tabia za watoto wanaokingana na sheria kutasaidia kupunguza idadi nyingi ya wahalifu kwa watoto na watu wazima.
Aidha alisema malengo ya Serikali ni kuona wakufunzi wanasimamia vyema watoto hao ili kuwa wanakaa mbali wanawake na wanaume na kuepuka vitendo vya udhalilishaji pindi litakapokamilika ujenzi wa jengo hilo .
Mapema Naibu Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa , Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Shamata Shaame Khamis amesema kazi kubwa ilio fanywa na mzee Karume wakishirikiana na wenzake kuhakikisha walipambana na kujitawala wenyewe .
Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua uwamuzi wa kuweka miundombinu imara na ilio bora kuhakikisha wanawaekea mazingira sawa wale wote watakao ingia kwenye magereza kwa kukiuka sheria .
Hata hivyo amewapongeza mafundi walio jitolea katika Chuo hicho kujenga jengo bila ya kutafuta mafundi wengine na kuweza kuokoa fedha za serikali katika ujenzii huo
Akitoa taarifa kwa niaba ya katibu mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa , Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Sida Himid amempongeza Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa usimamizi mzuri wa jengo hilo kwani kutasaidia kuondosha changamoto ya mlimbikano wa wanafunzi .
No comments:
Post a Comment