Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Awaapisha Viongozi Aliowateua Hivi Karibuni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.Ndg. Khatib Mwadin, hafla hiyo imefanyika Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi mbali mbali kushika nyadhifa baada ya kuwateuwa hivi karibuni.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali, Dk. Shein amemuapisha Khatib Mwadini Khatibu kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ame Burhan Shadhil kuwa Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali.


Miongoni  mwa waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na  Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu  Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee, Mawaziri, Spika wa Baraza la Wawakilishi,  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Washauri wa Rais pamoja na watendaji mbali mbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali Ndg.Ame Burhan Shadhil, hafla hiyo imefanyika Ikulu Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.