Habari za Punde

MUHIMBILI YASAMBAZA VAZI LA PPE KWA KAMATI ZA DHARURA JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Zuhura Mawona (kushoto) akimkabidhi Kaimu Mfamasia Mkuu Manispaa ya Kinondoni Bw. Oswen Sanga (Kulia)  mavazi ya kujikinga na Covid 19 yaliyoshonwa MNH.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Zuhura Mawona (kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu Manispaa ya Ilala  Dkt. Emily Lihawa (Kulia)  mavazi ya kujikinga na Covid 19 yaliyoshonwa MNH.


Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanza kusambaza  mavazi maalumu (coverall) ambayo ni sehemu ya mavazi ya watoa huduma (PPE) kuvaa ili kujikinga wakati wanatoa huduma wagonjwa wenye maambuki mbalimbali ikiwemo Covid 19 kwa kamati za dharura za Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari leo, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bi. Zuhura Mawona  amesema kuwa baada ya kujadiliana na Serikali bei elekezi itakuwa Tzs. 50,000 kwa kila vazi moja.

Manispaa ya Kinondoni imenunua mavazi 15 yenye thamani ya Tzs. 750,000, Ilala mavazi 20 yenye thamani ya Tzs. 1,000,000 huku Manispaa nyingine zikiendelea kulipia ili kupata mavazi hayo.

"Kwa sasa tunaanza na vituo vilivyopo katika Manispaa za jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine itafuata" amesema Bi. Mawona

Alisema kuwa mahitaji ni makubwa katika mikoa mbalimbali hivyo kwa sasa Muhimbili imejikita katika kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji.

Mapema wiki iliyopita Muhimbili ilizindua vazi hilo maalumu liloshonwa na wataalamu wa MNH kwa kutumia malighafi za ndani ya nchi lengo ikiwa ni kukabiliana na upungufu wa bidhaa hizo duniani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.