Habari za Punde

Virusi vya Corona: Kenya Yarekodi Visa Viwili.Katibu mkuu wa wizara ya Afya Mercy Mwangangi Jumamosi wagonjwa wapya ni Mkenya mmoja na mwingine ni raia wa kigeni.
Chanzo cha Habari.BBC News Swahili                                                                                    
Kumekua na kile kinachoonekana kama hatua inayotia moyo katika juhudi za kukabiliana na janga la virusi vya corona hususan vita dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo katika mataifa ya Afrika Mashariki ya Kenya na Rwanda.
Mataifa hayo yamerekodi kupungua kwa visa vipya vya maambukizi na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopona virusi hivyo wiki hii.
Nchini Kenya wagonjwa wawili ndio wamepatikana na maambukizi ya virusi vya corona katika muda wa saa 24 zilizopita, huku wagonjwa 11 wakitarajiwa kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona virusi hivyo nchini Rwanda.
Idadi hiyo inaifanya Kenya kuwa na jumla ya visa vya maambukizi kuwa 191, huku Rwanda ikisalia kuwa na wagonjwa 100 baada ya wagonjwa 18 kuthibitishwa kupona.


Kiwango kilichotangazwa cha visa vya corona Jumamosi ni cha chini cha maambukizi kutangazwa na Wizara ya afya nchini Kenya tangu kutangazwa kwa mara ya kwanza kwa maambukizi ya virusi hivyo tarehe 13 Machi ambapo mtu mmoja alitangazwa.
Katika tangazo lililotolewa na Katibu mkuu wa wizara ya Afya Mercy Mwangangi Jumamosi wagonjwa wapya ni Mkenya mmoja na mwingine ni raia wa kigeni.
Kisa kimoja kiliripotiwa katika Kaunti ya Nairobi huku kingine kikiripotiwa katika kaunti ya Mombasa, kufuatia kufanyiwa vipimo vya sampuli 491 za damu kwa muda wa saa 24.
Dokta Mwangangi, amesema kuwa raia wa kigeni hakua na historia ya kusafiri.
Ijumaa Kenya ilitangaza kuwa watu 10 waliokuwa wakipata matibabu ya virusi hivyo katika vituo vya kujitenga na hospitali ya Mbagathi wamepona na wataruhusiwa kwenda nyumbani, alisema Waziri wa afya Mutahi Kagwe.
Chanzo cha Habari 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.