Habari za Punde

RATIBA KAMILI YA MCHAKATO WA KUWAPATA WAGOMBEA WA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU1.0.     URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
NA
TAREHE
SHUGHULI/MAELEZO
1
15 – 30/06/2020
Kuchukua na kurejesha fomu. Mwisho wakurudisha fomu ni tarehe 30/6/2020 Saa 10:00 jioni.
2
15 – 30/06/2020
Kutafuta wadhamini Mikoani.
VIKAO VYA UCHUJAJI
3
06 – 07/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
4
08/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Taifa.
5
09/07/2020
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
6
10/07/2020
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa: Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa majina yasiyozidi matatu ya wanachama wanaoomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
7
11 - 12/07/2020
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.    2.0. URAIS WA ZANZIBAR
NA
TAREHE
SHUGHULI/MAELEZO
1
15 – 30/06/2020
Kuchukua na kurejesha fomu. Mwisho wakurudisha fomu ni tarehe 30/6/2020 Saa 10:00 jioni.
2
15 – 30/06/2020
Kutafuta wadhamini Mikoani.
VIKAO VYA UCHUJAJI
3
01 – 02/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.
4
03/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Zanzibar.
5
04/07/2020
Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kuhusu wanachama wanaoomba nafasi ya Rais wa Zanzibar.
6
09/07/2020
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya wanachama wasiozidi watatu wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar.
7
10/07/2020
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama kugombea Urais Zanzibar. 
8
11 - 12/07/2020
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Kuthibitisha  jina la mwanachama atakayesimama katika Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.


3.0.     MAMBO YA KUZINGATIWA NA KILA MGOMBEA
(i)         Kila mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lazima apate wadhamini 250 katika Mikoa 12 angalau Mikoa 2 kati ya hiyo iwe ya Zanzibar.

(ii)        Kila mgombea wa Urais wa Zanzibar ni lazima apate wadhamini 250 katika Mikoa isiyopungua mitatu, kati ya hiyo angalau Mkoa mmoja kutoka Unguja na mmoja kutoka Pemba.

(iii)      Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

(iv)      Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais wa Zanzibar.

(v)       Mwanachama haruhusiwi kumdhamini mgombea zaidi ya mmoja.

(vi)      Fomu ya udhamini ya wanachama ithibitishwe na Katibu wa CCM wa Wilaya kwa kupigwa muhuri wa chama wa Wilaya husika.

(vii)    Wanachama watakaomdhamini mgombea, uanachama wao uthibitishwe na Katibu wa CCM wa Wilaya husika.

(viii)   Kila mgombea atalazimika kuzingatia maadili ya Chama Cha Mapinduzi, masharti ya uongozi, sifa za wagombea na utaratibu wa kuomba uongozi kama ilivyofafanuliwa katika Kanuni za Uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya Dola, Kanuni za Uchaguzi na Kanuni za Uongozi na Maadili.

4.0    TAARIFA YA ZIADA
(i)      Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi ya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Kata/Wadi na Viti Maalum kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 watachukua na kurejesha fomu kati ya tarehe 14 na 17 mwezi Julai 2020. Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 17/07/2020 Saa 10.00 jioni.

(ii)     Taarifa rasmi ya mchakato wa kuwapata wagombea wa Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Kata/Wadi na Viti Maalum kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 itatolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi tarehe 11/07/2020.
        
MFULULIZO WA MATUKIO YA RATIBA YA MCHAKATO WA KUWAPATA WAGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WA NAFASI YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA RAIS WA ZANZIBAR KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020

MUDA/TAREHE
SHUGHULI/MAELEZO
15 – 30/06/2020
i)     Kuchukua fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar. 
ii)   Kutafuta wadhamini Mikoani.
iii)  Kurejesha fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar. Mwisho tarehe 30/6/2020 saa 10:00 jioni.
01 – 02/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.
03/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Zanzibar.
04/07/2020
Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kuhusu wanachama wanaoomba nafasi ya Rais wa Zanzibar.
06 – 07/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
08/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Taifa.
09/07/2020
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na majina ya wanachama wasiozidi watatu wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar.
10/07/2020
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama kugombea Urais wa Zanzibar na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa majina yasiyozidi matatu ya wanachama wanaoomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).
11 - 12/07/2020
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuthibitisha  jina  la mwanachama atakayesimama katika Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.