Habari za Punde

Mkutano Mkuu wa TAMWA -Zanzibar

Mkurugenzi wa TAMWA  Zanzibar  Dkt,Mzuri Issa akizungumza na Wanachama wa TAMWA Zanzibar wakati wa hafla ya mkutano Maalum uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Tamwa Zanzibar Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo. Akiwasilisha Ajenda za mkutano huo kwa Wajumbe wake. 
Rahma Sleiman ambae ni mwanachama wa TAMWA-ZNZ akitoa ushuhuda wa kesi za udhalilishaji kwa wanawake na watoto ambayo alifuatilia katika shehia ya Makunduchi mkoa wa kusini Unguja.
Baadhi ya Wananchama wa Chama cha Waandishi wa habari TAMWA-ZNZ wakiendelea na majadiliano katika mkutano mkuu wa Chama hicho ambao ulifanyika katika ofisi zake zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja.
Naibu Mkurgenzi wa Shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC) Bi.Nassra Mohamed akifafanya hoja wakati alipokua akichangia katika mkutano huo.
Mwandishi wa habari Kauthar Is-hak akichangia hoja baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ndani ya mkutano huo mkuu wa TAMWA-ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.