Na Jaala Haji Makame, ZEC
Mkuu
wa Mkoa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud alisema kurejewa kwa kazi ya
uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura kwa Mikoa yote ya Zanzibar ni
ishara moja wapo ya mafanikio makubwa kwa nchi yenye nia ya kuimarisha
demokrasia nchini.
Akizungumza
katika kituo cha Uandikishaji cha Bungi wakati akifanya ziara katika vituo vya
Uandikishaji alisema hatua hiyo imewajengea imani wananchi na kuondosha
malalamiko ambayo yangeweza kujitokeza katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi Mkuu.
Mhe.
Ayoub aliendelea kuwasisitiza wananchi ambao bado whawajaandikishwa na
kuhakikiwa taarifa zaao kushiriki kikamilifu katika kazi hiyo kwa salama na
utulivu wa hali ya juu.
Aliendelea
kusema kuwa ni jukumu la viongozi wa
vyama vya siasa kuhakikisha wanaendesha siasa za kistaarabu na kufuata Sheria, Kanuni, Miongozo na
taratibu zinazotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ili kufikia dhamira ya
kuendesha Uchaguzi Mkuu na kuufanya Uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
Aidha,
alisisitiza kuwa Viongozi wa Mikoa na
Wilaya wanajukumu la kuwahamasiha wananchi ili wajitokeze kwenda kujiandkisha
na kuhakikisha hali ya utulivu na Amani inakuwepo katika maeneo ya vituo vya
kujiandikisha.
“ sisi viongozi wa Mikoa na Wilaya tunajukumu la
kuwahamasisha wananchi waendelee kujitokeza kujiandikisha…………” alisema.
Nao
Mawakala wa vyama mbali mbali vya siasa katika vituo vya uandikishaji walitoa
ushauri kwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuendelea kutoa mafunzo kwa Wapiga
Kura licha ya mafanikio yanayopatikana hivi sasa katika vituo vya uandikishaji
na uhakiki wa taarifa za Wapiga kura ili wananchi waendelee kujitokeza zaidi.
Kazi
ya Uandkishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura imekamilika kwa mikoa yote
ya Pemba na Mkoa wa Kaskazini na Kusini kwa Upande wa Unguja ambapo kazi hiyo itaendelea
tarehe 9 na 10/6/2020 Wilaya ya Magharibi “A” na Wilaya ya Magharib “B” na
kukamilisha mzunguuko wa raatiba ya uandikishaji katika Wilaya ya Mjini tarehe
11 na 12/6/2020
No comments:
Post a Comment