Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais akutana na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia viongozi wakuu

Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakiishi inayosimamia viongozi wakuu Mheshimiwa Hassan Khamis Hafidh Kushoto ya Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman akielezea malengo ya Kamati yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia viongozi wakuu, walipofika ofisini kwake vuga kumsalimia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia viongozi wakuu, walipofika ofisini kwake vuga kumsalimia.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakiishi inayosimamia viongozi wakuu.

Picha na – OMPR – ZNZ


Na Othman Khamis, OMPR

Uwepo wa kamati za kudumu zinazosimamia viongozi wakuu katika baraza la wawakilishi, umesaidia kurahisisha utendaji kazi wa Serikali katika sekta mbali mbali nchini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah, ametoa kauli hiyo alipokutana na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia viongozi wakuu, walipofika ofisini kwake vuga kumsalimia.

Mh. Hemed alielezea Imani kubwa kwa kamati katika utekelezaji wa majukumu yao wakionyesha kuongeza uwezo wa kufanya vyema katika kusimamia majukumu yao kwa maslahi ya taifa.

Alisema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, imefarijika kwa ujio wa kamati hiyo iliyopata fura ya kutembelea taasisi mbali mbali za ofisi na kuwaahidi kuendeleza mashirikiano ili majukumu ya kamati yaweze kamilika vyema.

Mheshimiwa Hemed amewapongeza wajumbe wa kamati hiyo, kwa uwajibikaji wao, na kuwataka wawe tayari muda wote kuishauri na kuielekeza ofisi yake ili kuendana na kasi ya awamu ya nane ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Nae Mjumbe wa kamati hiyo, ambae pia ni Muwakilishi wa Jimbo la Mfenesini, Mhe. Machano Othman Said kwa niaba ya kamati hiyo, amempongeza Makamu wa Pili wa Rais kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

Kamati imeridhika na Mtendaji Mkuu huyo wa Shughuli za Serikali jinsi alivyoanza utendaji wake kwa kasi katika kusimamia muelekeo wa awamu ya nane wa kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Mhe. Machano alishauri ni vyema kwa Serikali kuiangalia vyema sekta ya habari nchini hasa magazeti, ili machapisho yake yasaidie  kuwafikishia habari wananchi wa Zanzibar kwa urahisi zaidi.

Kamati ya Baraza la Wawakiishi inayosimamia viongozi wakuu chini ya mwenyekiti wake Mheshimiwa Hassan Khamis Hafidhi, ina ya wajumbe wanane.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.