Hafla hiyo ya futari iliyoandaliwa na Rais Dk. Mwinyi kwa ajili ya wananchi wa Mkoa huo wa Kusini Unguja ilifanyika katika ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliopo katika Kampasi ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Tunguu, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali, dini, vyama vya siasa pamoja na wananchi wa Mkoa huo.
Akitoa shukurani zake kwa wananchi waliohudhuria futari hiyo, Alhaj Dk. Mwinyi alisisitiza haja ya kuendeleza amani na maendeleo ili Zanzibar izidi kupiga hatua.
Alhaj Dk. Mwinyi alitoa shukurani kwa wananchi wote waliohudhuria futari hiyo aliyowaandalia na kutoa shukurani kwa kukubali na kuhudhuria muwaliko wake huo.
Aidha, Alhaj Dk. Miwnyi alieleza kwamba ameona haja ya kuandaa furati hiyo ili aweze kuungana na wananchi wa Mkoa huo katika mwezi huu mtufu wa Ramadhani.
Katika shukrani zak hizo, Alhaj Dk. Mwinyi alieleza utaratibu wake ambao ameuanza wa kufutari na wananchi wa mikoa ya Unguja na Pemba ambapo kesho Jumaatatu ya Machi 03.2021 anatarajia kufutari na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Wakati huohuo, nae Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi kwa upande wake aliungana na viongozi wanawake wa kitaifa pamoja na wananchi wa Mkoa huo wa Kusini Unguja katika futari hiyo maalum aliyoianda Dk. Mwinyi katika ukumbi huo.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment