Habari za Punde

Mhe Hemed akutana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Udhibiti wa Nishati Afrika Mashariki Dk. Geoffrey Mabea

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Udhibiti wa Nishati Afrika Mashariki aliambatana na viongozi kutoka Mamlaka ya udhibiti wa Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) waliofika Afisini kwake Vuga kujitambulisha.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Udhibiti wa Nishati Afrika Mashariki Dk. Geoffrey Mabea akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais Andiko la Mradi  kwa ajili ya Ujenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Udhibiti wa Nishati Afrika Mashariki ambayo inatarajiwa kujengwa Nchini Tanzania.


Na Kassim Abdi, OMPR

Jumuiya ya Wadhibiti wa huduma ya Nishati ya Afrika  Mashariki wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kuunga mkono jitihada za ujenzi wa  Taasisi ya Mafunzo ya Udhibti wa Nishati  Afrika Mashariki ambayo inatarajiwa kujengwa Nchini Tanzania.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wadhibiti wa Huduma za Nishati Afrika Mashariki Dk. Geoffrey Mabea  alieleza hayo wakati alipofanya mazungumzo pamoja kujitambulisha kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Alisema Jumuiya yao ya Udhibiti wa Nishati katika Ukanda wa Afrika Mashariki imepanga kujenga taasisi itakayotoa mafunzo kwa watu wake nchini Tanzania kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kitaalamu watendaji kutoka Nchi wananchama.

Dk. Geoffrey alimuleza Mhe. Hemed kuwa, hatua hatua hiyo itasaidia kuitangaza Tanzania na Afrika Mashariki  kwa kuwaanda wataalamu wengi ambao watasaidia Afrika na dunia kwa ujumla katima masuala mazima ya huduma za nishati.

Alifafanua kwamba Jumuiya ya Udhibiti wa Nishati kwa Nchi za Afrika Mashariki ambayo Makao Makuu yake yapo Jijini Arusha tayari imekwisha taarisha masuala ya msingi kwa ajili ya utekelezaji wa azma hiyo ambapo viongozi wa Jumuiya hiyo wanaendelea kutafuta eneo mahususi kwa ajili ya ujenzi wa Taasisi hiyo ya Mafunzo.

Nae Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla aliwapongeza viongozi wa Jumuiya hiyo kutokana na juhudi wanazozichukua katika kuimarisha udhibiti wa Huduma za Nishati kwa Afrika Mashariki na ameahidi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano.

Mh. Hemed alieleza kuwa ipo haja kwa Jumuiya hiyo kuangalia namna bora ya utoaji wa huduma zinazoendana na mabadliko ya teknolojia duniani ili kurahisisha zaidi gharama za uwendeshaji wa huduma hizo.

Katika hatua nyengine Makamu wa Pili wa Rais aliwaomba viongozi wenye dhamana ya usimamizi wa Jumuiya hiyo kuangalia namna bora kuimarisha viwango vya nishati kwa kujifunza Zaidi kutoka mataifa yalioendelea kwa lengo la kutumia mbinu mpya za kiuendeshaji.

Nchi zote ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Kauli moja wamekwisha kukubaliana Taasisi hiyo ya Mafunzo ya udhibiti wa Nishati kujengwa Nchini Tanzania.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.