Habari za Punde

Ukatili wa kijinsia na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto bado waendelea

Mwenyekiti Tume ya haki za Binaadamu  na Utawala Bora Mathew Mwaimu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mafunzo juu ya haki za Binaadamu yatakayoshirikisha wananchi 400 wa sehemu mbalimbali Unguja na Pemba huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Mwenyekiti Tume ya haki za Binaadamu  na Utawala Bora Mathew Mwaimu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mafunzo juu ya haki za Binaadamu yatakayoshirikisha wananchi 400 wa sehemu mbalimbali Unguja na Pemba huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Na  Khadija Khamis –Maelezo,   

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Methew P.M. Mwaimu amesema licha ya jitihada za serikali na wadau mbalimbali, kupiga vita vya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto bado unaongezeka nchini .


Hayo ameyasema  katika ukumbi wa sanaa rahaleo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali .


Amesema taarifa za ongezeko la vitendo vya udhalilishaji kwa watoto hususan wa jinsia ya kiume ni kubwa kwa Zanzibar jambo ambalo  linaashiria  maisha ya watoto kuwa hatarini.


Aidha amesema mnamo mwezi Januari 2020 matukio 116 ya watoto kufanyiwa  ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yaliripotiwa katika vituo vya polisi na matukio mengine 122 yaliongezeka kuripotiwa kwenye vituo hivyo.


Mwenyekiti  huyo amesema tume ya haki za binaadamu na utawala bora imeona kuna umuhimu mkubwa wa wadau kuongeza jitihada ya kutoa elimu ili kuengeza uelewa wa masuala ya haki za binaadamu na utawala bora kwa makundi mbali mbali ya umma .


Alifahamisha kuwa elimu hiyo wataopewa ni masheha wa shehia mbali mbali ,viongozi wa dini pamoja na wanawake na watoto.


Alieleza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kubadilishana maarifa na uzoefu kwa lengo la kukomesha tatizo hilo nchini na kuamini kwamba elimu hiyo itawawezesha viongozi na wananchi kutambua haki zao na kutimiza wajibu wao kwa ufanisi zaidi kwa kuzingatia haki za binaadamu na misingi ya utawala bora .

Pia amesema viongozi na wananchi hao watakaopata mafunzo hayo watakuwa chachu katika jamii ya kuwaelimisha wengine mifumo sahihi ya kutoa taarifa na kudai haki zao zinapokuwa zimevunjwa pamoja na mambo mengine .


“elimu tunayoitoa ni ya hatua moja muhimu ya kufikia ndoto ya tume ya kuwa na jamii yenye kuheshimu haki za binaadamu, misingi ya utawala bora pamoja  na utu wa mtu ,”alisema Mwenyekiti  huyo.


Aidha alisema tume inaahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote katika kuhakikisha kuwa haki za wanawake na watoto zinalindwa ,zinatunzwa,na kutetewa kote nchini .


Kauli mbiu ya tume hiyo ni“ PAZA SAUTI KOMESHA UKATILI NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA DHIDI YA WATOTO”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.