Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ahutubia katika mkutano wa ufunguzi wa Maonesho ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika, akimuwakilisha Rais Mhe Samia Afrika Kusini

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa alipowasili katika ukumbi wa ICC Arena  Jijini Durban kuhudhuria Mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika, hafla jiyo imefanyika leo 15-11-2021 Jijini Darban Afrika Kusini.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kubadilishana mawazo na Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa alipowasili katika Jengo la Mikutano la la Kimataifa la ICC Arena Jijini Durban Afrika Kusini, mkutano huo umefunguliwa leo 15-11-2021.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe.Olusegun Obasanjo, alipowasili katika jengo la Mikutano la Kimataifa la ICC Arena Jijini Durban Afrika Kusini, kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan,
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo wakati wa maongezi yake na Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa, wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano kabla ya kuaza kwa mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Arika uliofanyika katika ukumbi wa ICCArena Jijini Durban, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. Uliofanyika leo 15-11-2021.
WASHIRIKI wa Mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika, wakipiga makofi wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa ICC Arena Jijini Durban Afrika Kusini.
WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban na (kushoto kwake) Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe.Exaud Kigahe wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika uliofanyika katika ukumbi wa ICC Arena Jijini Durban Afrika Kusini, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia hutuba ya Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika, wakati Rais wa Afrika Kusini Mhe Cyril Ramaphosa akihutubia mkutano huo wa ufunguzi (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa ICC Arena Jijini Durban Afrika Kusini.
MKURUGENZI Idara ya Diplomasia ya Uchumi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Edwin Lutageruka,akifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika mkutano ufunguzi wa Maonesho ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, uliofanyika leo 15-11-2021. Katika ukumbi wa mikutano wa ICC Arena Jijini Darban Afrika Kusini.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika mkutano wa ufunguzi wa Maonesho ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, ulifanyika katika ukumbi wa ICC Arena Jijini Durban Afrika Kusini leo 15-11-2021.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe.Omar Said Shaban, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa maonesho ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa ICC Arena Jijini Darban Afrika Kusini leo 15-11-2021.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.