Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Amewata Waumini wa Dini ya Kiislam Kuwa na Mipango Madhubuti Kutimiza Wajibu wa Uislam.

MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman akikata utepe kuashiria ufunguzi wa msikiti wa Aisha Mohammed Ismail huko Mwera Mkwajuni leo kabla ya swala ya Ijuma. Kushoto kwa makamu ni Naibu Muft Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi na anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Shrika la Annour Charatable Organzation for the need Sheikh Nadir Mahfudh.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Alhaj Othman Maoud Othman akikabidhi Funguo za Masjid Aisha Mohammed Ismal kwa imamu Mkuu wa Msikiti huo Sheikh Abrahaman  Ali Mussa  mara baada ya ufunguzi rasmi uliofanyika leo huko Mwerra Mkwajuni Magharib A. Kulia kwa makamu ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi na Kulia ni  Mkurugenzi wa Shrika la Annour Charatable Organzation for the need Sheikh Nadir Mahfudh. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Alhaji Othman Masoud, amesema ni muhimu kwa waumini wa dini ya kiislamu nchini kuwa na mipango madhubuti katika kutimiza wajibu wa uisalamu na kutekeleza ibada ya dini yao.

Mhe. Othman ameyasema hayo leo alipowasalimia waislam baada ibada ya Swala ya Ijumaa iliyoambatana na ufunguzi wa Masjid Aisha Bint Mohammed Issmail huko Mwera Mkwajuni wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja.

Amesema kwamba ni lazima waislamu wazifanye nyumba za ibada kuwa ni taasisi muhimu mashaurinano na mafumzo kwa vizazi na jamii kwa jumla kwa kuweka mipango na utaratibu bora kupitia njia ya misikiti kwa nia ya kuendeleza ibada ya uislamu na jamii kwa jumla.

Aidha ametaka waislamu kuendeleza uislamu wao kwa kuwa na utamaduni wa kutoa na kuchangia mali walizoruzukiwa kama njia sahihi ya uendelezaji wa dini yao na kwamba kufanya hivyo ndio yanayojenga usialam na jamii kubaki na mshakamano na kuendeleza sifa bora ya usialamu.

Ameikumbusha jamii kufanya ibada sambamba na kutoa mafunzo bora kwa vijana yanayojenga maadili mema yanayotokana na muongozo wa ili kupata viongozi bora wa hapo baadae watakaoweza kusaidia vyema nchi yao.

Aidha amewakumbusha waumini wa dini ya Kislamu na jamii kwa jumla kutofanya israfu katika matumizi ya rasilimali mbali mbali yakiwemo maji kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maamrisho ya mola muumba.

Mapema khatib wa msikiti huo katika swala ya Ijuma Sheikh Iddi Hussein Iddi, amekumbusha umuhimu wa waislam kuendeleza nyumba za ibada kama ilivyoelekezwa na mola muumba yakiwamo masuala ya utaoaji wa mafunzo na kufanya mashauri mbali mbali yanayohusu jamii.

Naye Mkurugenzi wa shirika la Alnour charateble Organization for the Need, Sherikh Nourdeen Makhafoudh amesema kwamba , shirika lake litaendelea kusaidia juhudi mbali mbali za waumini na wananchi kwa jumla katika kukuza na kuendeleza uislamu nchi kwa ujenzi wa misikiti, taasisi za mafunzo , kusaidia mayatima pamoja na jamii kwa jumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.