Habari za Punde

Ni Simba au Azam fainali ya Mapinduzi Cup leo

 NA ABOUD MAHMOUD

TIMU za soka ya Simba na Azam FC leo zinashuka dimbani leo kuwania ufalme wa kombe la Mapinduzi mwaka 2022.

Mtanange huo utaanza majira ya saa 2:15 usiku katika uwanja wa Amaan ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ataongoza mashabiki kushuhudia mchezo huo.

Wakizungumzia mchezo huo  viongozi wa timu hizo kila mmoja alijinata kushinda na kubeba ubingwa.

Mtendaji mkuu wa timu ya Simba Barbara Gonzalez alisema kikosi chao kipo kamili kupambana na timu yoyote, ili kuhakikisha inachukua ubingwa wa kombe hilo kwa mara ya nne.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.