Habari za Punde

Umoja wa madaktari Zanzibar watoa huduma za Afya kwa wananchi mbalimbali wa wilaya ya kati

Madaktari kutoka umoja wa madaktari Zanzibar wakiwapatia huduma za Afya wananchi mbalimbali  wa  wilaya ya kati katika zoezi la matibabu bure liloratibiwa na baraza la Mji kati huko kituo cha Afya Kidimni Wilaya ya kati Mkoa wa  Kusini  Unguja
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid akitembelea kituo cha Afya Kidimni wakati wa zoezi la utowaji wa huduma za Afya bure kwa wananchi wa Mkoa huo ,zoezi hilo lililoratibiwa na baraza la Mji Kati  litadumu  kwa muda wa siku mbili (19-20.03.2022).
Wananchi wa Shehia mbalimbali za Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja wakisubiri kupatiwa  huduma za Afya kutoka kwa madaktari mbalimbali wa Umoja wa Madaktari , wakati wa zoezi la utowaji wa huduma za Afya bure katika  kituo cha Afya Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la utowaji wa huduma za Afya bila malipo katika Mkoa wake ,mara baada ya kufika katika Kituo cha Afya Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja  kuangalia  zoezi hilo linavyoendelea
Mkurugenzi kinga na Elimu ya Afya dkt.Salum Slim akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umoja wa madaktari waliojitolea kuwahudumia wananchi wa mkoa Kusini  Unguja katika zoezi maalum la kuwapatia huduma za matibabu bila malipo ndani ya kituo cha Afya kilichopo  Kidimni wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ,zoezi hilo liliratibiwa na Baraza la Mji Kati
Mkurugenzi Baraza la Mji Kati Salum Mohammed Aboubakar akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la upatikanaji wa huduma za Afya bila malipo katika kituo cha Afya Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ,wakati zoezi hilo likiendelea .
Mwandishi wa Habari gazeti la  Zanzibar leo ambae pia ni mkaazi wa kibele Mkoa wa Kusini Unguja  Madina  Issa akipatiwa huduma ya Afya ya macho katika Kituo cha Afya Kidimni wakati wa zoezi la utoaji wa huduma bila malipo kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja liloratibiwa na Baraza la Mji Kati.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)dkt.Ibrahim kabole akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Kituo cha Afya Kidimni Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –ZANZIBAR.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.