Habari za Punde

Mhe Hemed akutana na Waziri wa nchi wa UAE Sayyid Maythaa Al Shaamy

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeupongeza Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) kwa kuendelea kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kufadhili miradi mbali mbali ya Maendeleo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Umoja wa Falma za Kiarabu (U.A.E) ukiongozwa na Waziri wa Nchi wa U.A.E Sayyid Maythaa Al Shaamy Afisini kwake Vuga Jijini Zanzibar. 

 

Ameeleza kuwa Waziri huyo wa Nchi wa UAE ameihakikishia SMZ kuendeleza mashirikiano katika nyanja tofauti ikiwemo miradi inayowalenga Wanawake na Mayatima.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Umoja wa Falme za Kiarabu unafahamu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwatumikia Wananchi wake.

 

Sambamba na Mhe. Hemed amemueleza Waziri huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi imeshatoa miongozo ya kukaribisha Taasisi mbali mbali za ndani na za Nje ya Nchi ili kuja kuunga mkono Juhudi hizo.

 

Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed amemuhakikishia Waziri Maythaa kuwa SMZ itasimamia Misaada wanayoitoa kwa kuwafikia walengwa kama walivyokusudia.

 

………………

Abdulrahim Khamis

Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

04/07/2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.