Habari za Punde

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Stergomena Awasili Wizarani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokelewa na  Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipowasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na mmoja wa watumishi wa Wizara alipowasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk  na Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.), Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara.

Dkt. Tax ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 02 Oktoba 2022 na kuapishwa tarehe 03 Oktoba 2022 Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

Dkt. Tax amechukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula baada ya Mhe. Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri. 

Akizungumza baada ya kuwasili katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Mhe  Dkt. Tax amesema atashirikiana na watumishi wote wa Wizara katika kila ngazi ili kuhakikisha malengo ya Wizara yanatekelezwa kikamilifu.

“Nipo tayari kufanya kazi na nyinyi, na kujifunza kutoka kwenu ili kutekeleza majukumu yangu….. Taasisi yoyote ili iweze kufanikiwa lazima ifanye kazi kwa pamoja na kuwa na ushirikiano,” amesema Dkt. Tax.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk  wakimsikilza Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine alipokuwa akimkaribisha Dkt. Tax katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine katika picha ya pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine, Wakurugenzi wa Idara mbalimbali katika Wizara na baadhi ya watumishi katika picha ya pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.