RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia Balozi wa Shirikisho la Somali Nchini Tanzania.Mhe.Zahra Ali Hassan,alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo na kujitambulisha leo 23-11-2022.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Shirikisho la Somali Nchini Tanzania Mhe. Zahra Ali Hassan, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 23-11-2022, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Balozi wa Shirikisho la Somali Nchini Tanzania Mhe. Zahra Ali Hassan, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 23-11-2022, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Balozi wa Shirikisho la Somali Nchini Tanzania Mhe. Zahra Ali Hassan, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 23-11-2022,alipofika kujitambulisha.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi amezungumza Balozi wa Shirikisho la Somali nchini Tanzania, Ikulu
Zanzibar aliefika kwa ajili ya kujitambulisha.
Dk.
Mwinyi amewaomba wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Somalia kuja Zanzibar kwa
ajili ya kuwekeza katika sekta mbali mbali, ikiwemo uanzishaji wa Nyumba za makaazi.
Alisema
Zanzibar ina fursa nyingi za Uwekezaji, huku akibainisha miradi ya uanzishaji wa nyumba za makaazi
kuwa ni eneo lenye fursa pana kwa ajili ya kuwekeza.
Aidha, alipongeza
uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Somalia na Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla, ambapo wananchi wa nchi hizo wamekuwa na maingiliano ya
muda mrefu pamoja na kushirikiana katika nyanja mbali mbali za kijamii pamoja
na kibiashara.
Nae,
Balozi wa Shirikisho la Somalia nchi Tanzania Zahra Ali Hassan alishukuru
mashirikiano makubwa yaliopo kati ya wananchi wa nchi mbili hizo, huku
akibainisha azma ya wananchi wa Somali kuendeleza ushirikiano huo kwa kuwekeza
katika miradi mbalimbali pamoja na kuimarisha biashara.
Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano
Ikulu Zanzibar.
No comments:
Post a Comment