Habari za Punde

Maghala ya kuhifadhi gesi yatahadharishwa

 Na Khadija Khamis- Maelezo, Zanzibar .


Mkuu wa Devisheni ya  Uperesheni wa Huduma za Kibinaadamu Haji Faki Hamduni amewataka wamiliki wa maghala yanayohifadhi  mitungu ya gesi kufuata utaratibu wanaopangiwa na mamlaka husika ili kuepusha madhara ya maafa .


Akiyasema hayo katika ghala la kuhifadhi  gesi ijitimai Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B wakati wa ziara maalumu  ya ukaguzi wa mazingira hatarishi katika maeneo tofauti ya Mkoa Mjini Magharibi .


Amesema kuwa hakuridhishwa na baadhi ya maghala hayo kutokana na mazingira yaliyopo katika makaazi ya watu na hali ya usalama uliopo ni mdogo.


Aidha alisema pindipo watapuuza taratibu walizopangiwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya maghala hayo kwa kunusuru madhara ambayo yataweza kujitokeza.


Wakati huo huo walitembelea Skuli ya Sekondari ya Mwera Regeza Mwendo na kuangalia hali ya mazingira ya kambi zinazokaa wanafunzi  ili kuweza kujua hali halisi ya usalama wao .


Ukaguzi wa kuangalia mazingira hatarishi kwa jamii umewashirikisha Wafanyakazi kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa,Afisa kutoka ZURA, Afisa Mazingira, Afisa Afya pamoja na Afisa Habari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.