13.11.2022
IRINGA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussin Mwinyi ametoa wito kwa washiriki wa
Maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini 2022 yaliyofanyika Mkoani Iringa Tanzania
Bara kuitumia vyema fursa ya kuwepo maonesho hayo kupanua wigo wa kibiashara sambamba na
kuimarisha ushirikiano katika kukuza sekta hiyo nchini.
Mhe. Dk. Mwinyi ameyasema hayo Mkoani
Iringa katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman katika ufungaji rasmi wa Maonesho ya Utalii
yaliyopewa jina la Karibu Kusini yaliyofanyika
huko Iringa Tanzania Bara.
Aidha Dk. Mwinyi amewahimiza viongozi na watendaji katika
ngazi mbali mbali na wananchi kwa jumla kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais
wa Jamhumuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan katika kutangaza
na kukuza sekta ya utalii hapa nchini na kwengineko duaniani.
Amefahamisha kuwa kupitia program ya
Royal Tour Mhe. Rais amewafungulia watanzania fursa kubwa ya kuendeleza sekta
ya Utalii nchini sekta ambayo inatoa mchango muhimu katika kukuza uchumi wa
Tanzania , ustawi wa jamii pamoja na uhifadhi wa mazingira.
Dk . Mwinyi amewahimiza Watanzania
kuvitembelea vivutio vya Utalii vilivyopo kusini mwa Tanzania ili kutekeleza
kwa vitendo kauli mbinu ya nchi ya
uhifadhi wa maliasili ambayo ni hazina muhimu isemayo ‘ tumerithishwa
tuwarithishe’
Aidha Mhe. Mwinyi amesema kwamba
Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vyua Utalii vikiwamo vya asili na historia, ikiwemo misitu ya
asili inayohifadhi na viumbe wasiopatikana mahali popote duniani ispokuwa
Tanzania sambamba na tamaduni na hiostoria zenye nguvu sana duniani ikiwemo ile
ya Chifu Mkwawa , ngome ya Kolenga , maporomoko
ya maji , maziwa pamoja na milima yenye muonekano na mandhari za kuvutia
kiutalii.
Amesema kwa upande wa Zanzibar kuna
fukwe za aina yake , mji mkongwe , maeneo ya historia viongo na mazao ya aina hiyo sambamba na kuwepo mandhari bora na tulivu
ambapo wageni mashuhuri na watalii
kutoka kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika kwao ni vivutio vikubwa vya kuja kuvitembelea.
Mhe. Mwinyi ameeleza kwamba vivutio
hivyo vilivyopo Tanzania kabla ya
maradhi ya uviko 19 mapato yatokanayo na sekta ya utalii yalifikia dola
za Marekabili bilioni 2.6 na kuchangia wastani wa asilimia 17 ya pato la
taifa ambazo ni sawa na asilimia 25 ya
pato la fedha za kigeni na kuzalisha
ajira zaidi ya milioni moja na lakini sita.
Amefahamisha kwamba mafanikio hayo ni
matokeo ya juhudi za serikali kwa
kushirikiana na sekta binafsi kuendeleza sekta hiyo ikiwa ni pamoja na
kulifufua shirika la Ndenge Tanzania ATCL
ili kuimarisha sekta ya usafiri kwa
watalii na wageni mbali mbali .
Aidha amesema kwamba Tanzania
imefanikiwa kuwa mwenyeji wa mikutano na matukio mbali mbali ya kimataifa ikiwa ni mafanikio ya zao la
kuanzisha mpan go na program za utalii
wa kimkakati katika sekta ya Utalii
ambapo yamesaidia sana katika kuitangaza Tanzania na kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea
nchi.
Amesema maonesho ya utalii ya Karibu Kusini 2022 yatakuwa na manufaa makubwa kwa kukuza utalii
na kuongeza idadi ya wataali ambapo mwaka huu wa 2022 kuanzia Januari hadi
Septemba Tanzania imetembelewa na
watalii wa kimataifa wapatao moja elf
thelathini nanne na mia na Themanini (1,034180).
Naye waziri wa Maliasili na Utaliii wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Balozi Dk. Pindi Chana, amesema
kwamba maonesho hayo yatachangia sana katika kuiarisha jitihada kuitangaza
Tanzania katika kukuaza uwekezaji kwenye
sekta ya utalii.
Amesema kwamba hatua hiyo inatikana
na ukweli kwamba bado Tanzania inahitaji kufanya juhudi za kuionesha
duania maeneo na vivutio mbali mbali
vile vya maumbile na vya historia vilivyopo nchini Tanzania kwa lengo la kukuza
maendeleo ya biashara ya utalii ikiwa ni hatua ya kuingamkono Jitihada za Rais
Samia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa huo Mhe.
Halima Omari Dendego akitoa salamu za Mkoa huo amasema kwamba kufanikiwa
kwa maonesho hayo muhimu ni maotokeo ya
juhudi kubwa za ushirikiano wa viongozi mbali mbali wa Miko kumi ya Kanda ya
Kusini katika kuendeleza jitihada za kimarisha utalii nchini. .
Maoneyo ya Utalii ya Karibu Kusini
2022 yaliyofanyika katika eneo Keisa Kilolo Iringa kuanzia tarehe tisa hadi 13
mwaka huu 2022 yamewashirikisha waoneshaji
wa sekta ya Utalii wa ndani nanje ya Tanzania na yamefungwa rasmi leo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Othman Masoud Othman kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Mwinyi.
Mwisho.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo cha habari leo tarehe 13.11.2022.
No comments:
Post a Comment