MKE wa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation
(ZMBF), Mama Mariam Mwinyi amesema taasisi hiyo inatekeleza kwa vitendo Sera ya
Uchumi wa Buluu ya Serikali ya awamu ya nane ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mama
Mariam Mwinyi aliyasema hayo kwenye ofisi za taasisi hiyo, Migombani Wilaya ya Mjini
alipozungumza na ugeni kutoka jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi, UVCCM waliofika kumtembelea.
Alisema
tokea kusajiliwa kwa ZMBF Febuari 19 mwaka jana ambayo kwasasa imetimiza mwaka
mmoja, wanajivunia mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Sera za Serikali kwa
vitendo hasa sera ya Uchumi wa Buluu.
Alisema
dhana ya Uchumi wa buluu kwa taasisi ya ZMBF imejikita kwenye harakati za
kuwasaidia na kuungamkono juhudi za kinamama wanaojitoa kupigania maendeleo ya
kiuchumi kupitia matunda ya baharini.
Alisema
ZMBF imefanikiwa kuwafikia kinamama wengi Unguja na Pemba wanaujishughulisha na
kilimo cha mwani na kueleza asilimia 90 ya ukulima huo hushirikisha kinamama.
Alisema
katika jitihada za kuwaungamkono, ZMBF imewasaidia vifaa mbalimbali vya uvuvi
kinamama hao ikiwemo boti zenye mashine, viatu vya kuvalia baharini, mashine za
kusagia mwani zenye uwezo wa kusaga mwani mwingi kwa wakati hali iliyowasaidia
kinamama hao kuongeza ufanisi wa kazi zao na kuwaongezea kipato kwa kukabiliana
vyema na soko la bidhaa hiyo.
“Kutokana
na mabadiliko ya tabianchi, siku hizi kinamama hufanya shughuli za kilimo cha
mwani nje kidogo na usawa wa bahari kutokana na kina cha maji ya bahari
wanayolimia tofauti na zamani walilima maeneo karibu hivyo, ZMBF imeona haja ya
kuwasaidia vifaa kimama hao, hususani boti zenye mashine kwaajili ya kuvukia na
shughuli zao za baharini pamoja na viatu kwa usalama wanapokua baharini”
Alifafanua Mama Mariam.
Mama
Mariam ambae pia ni Mlezi wa Matembezi ya UVCCM ya Mapinduzi ya Zanzibar
aliwaeleza vijana hao kwamba pia ZMBF imejita kwenye harakati za utunzaji mazingira
kwa kuishajihisha jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha
usafi.
Alisema
katika harakati hizo, ZMBF inajishughulisha na utengenezaji wa taulo za kike za
kufua na kuhifadhi baada ya matumizi, ambazo huwasaidia wasichana mashuleni
hasa wale wanaotoka kwenye mazingira magumu ambao hawana uwezo wa kuhimili
taulo za kawaida.
Aidha,
alieleza taulo za kawaida ambazo hutupwa baada ya matumizi huchangia wimbi la
uchafuzi wa mazingira na kueleza kwama nyingi husalia kutupwa baharini na
kuathiri viumbe vya bahari.
Akizungumzia
tatizo la magojwa yasiyoambukiza yanayoendelea kuiathiri jamii, Mama Mariam
Mwinyi alieleza ZMBF imekua ikishajihisha jamii kufanya mazoezi na kuambatana
nao kwenye makongamano mbalimbali yanayohusisha matembezi ya hiari ambayo
husaidia jamii kufanya mazoezi ili kujiepusha na kujinginga na maradhi hayo
yakiwemo, presha, kisukari matatizo ya moyo na saratani.
Kuhusu
suala la udhalilishaji wa kijinsia, alieleza ZMBF inakerwa zaidi na vitendo hivyo
ambavyo huwaathiri zaidi wanawake na Watoto, alisema licha ya harakati nyingi
zinazofanya na taasisi hiyo kwa kuwagusa moja kwa moja kinamama, vijana,
wasichana na Watoto suala la udhalilishaji wamekua wakilikemea kwa nguvu zote
na kulipiga vita.
Katika
hatua nyengine Mlezi huyo wa UVCCM aligusia matayarisho ya miaka 60 ya
Mapinduzi ya Zanzibar na kuwataka vijana hao kufanya maandalizi ya aina yake
kwani vijana ni sauti ya Chama hasa kwenye kuimarisha mustakabali wa maendeleo
na mabadiliko kwenye nyanja zote za siasa, uchumi na jamii.
“Kuna
haja ya kukaa chini na kufikiria namna kutakavyoadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi
ya Zanzibar yawe ya aina yake, muje na fikra tofauti, UVCCM ije na kitu tofauti
sababu vijana ndio injini ya Chama” aliwashajihisha vijana hao.
Naye, Makamu
Mwenyekiti UVCCM taifa, Ndg. Rehema Sombi Omari (MNEC) kwa niaba ya ugeni
alioambatana nao, waliipongeza ZMBF kwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa kwa kipindi
cha muda mfupi pia waliahidi kuwa balozi wazuri wa kukitangaza Chama na kupaza
sauti zao kwa umma kuyasemea mazuri yote yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar inayoongozwa na Dk. Mwinyi na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania chini ya uongozi imara wa Dk. Samia Suluhu Hassan.
Akilizungumzia
jengo la UVCCM, ofisi ya Jimkana, Zanzibar alisema wanatarajia kulifanyia maboresho
makubwa ili kueka alama kwa vizazi vijavyo kwamba UVCCM 2022 – 2077 ilifanya
makubwa wakati wake.
No comments:
Post a Comment