Habari za Punde

Wananchi wa Jijini la Zanzibar Wajumuika katika Maziko ya Mwanachuoni Maarifu Zanzibar Marehemu Sheikh. Said Mahmoud Abdulrahim

Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi akiongoza Viongozi wa Serikali na Wananchi katika Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Mwanachuoni maarufu Zanzibar Sheikh Said Mahmoud Abdulrahim, iliyofanyika katika Masjid Ngamia Welezo Wilaya ya Mjini Unguja na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe jana 25-5-2023.

Viongozi mbali mbali wa Dini na Serikali wamehudhuria katika Mazishi ya Mwanachuoni nchini Sheikh Said Mahmoud Abdulrahim aliesaliwa Msikiti Ngamia Welezo na kuzikwa Makaburi ya Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi. 

Viongozi mbali mbali wamehudhuria katika katika mazishi hayo wakiongozwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman masoud Othman.

 

Viongozi wengine waliohudhuria katika Mazishi hayo ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya saba Alhajj Dkt. Ali Mohamed Shein, Jaji Mkuu wa Zanzibar Alhajj Khamis Ramadhan Abdallah, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi.

 

Wengine ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Ame Chum, Viongozi mbali mbali wa Dini na Serikali, Wanafamilia, na Wananchi mbali mbali wa Zanzibar.

 

Akisoma Wasfu wa Marehemu Sheikh Muhiddin Ahmad Khamis (Maalim Siasa) ameeleza kuwa marehemu amepata Elimu ya Msingi na Sekondari katika Skuli ya Darajani, Chuo cha Kiislamu na Elimu ya juu amesoma nchini Saudi Arabia.

 

Katika uhai wake marehemu Sheikh Said Mahmoud Abdulrahim amewahi kuwa Kadhi wa Wilaya, Mwalimu Skuli ya Jang’ombe,  Mwalimu wa Tafsiri ya Quran Mskiti wa Sheikh Ameir Tajo, Mskiti wa Mchangani Mjini Unguja, Baladul Amiin Kilimahewa.

 

Marehemu Sheikh Said Mahmoud Abdulrahim amefariki jana Jumatano na kuzikwa leo viunga vya Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi.

 

Marehemu ameacha Kizuka Mmoja na watoto wawawili.

 

Innaa Lillaahi wainnaa Ilaihi Raajiun.


Abdulrahim Khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

25/05/2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.