Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameagwa rasmi na mwenyeji wake Mke wa Rais wa Burundi Mhe.Mama Angeline Ndaishimiye baada ya kukamilisha ziara yake ya siku 3 ya kushiriki Mkutano wa viongozi Wanawake uliofanyika Burundi.
Mama Mariam amerejea Zanzibar leo tarehe 12 Oktoba 2023.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)Mhe. Mama Mariam Mwinyi amefanya Ziara kutembelea benki ya CRDB tawi la Burundi, Bujumbura.
Katika nasaha zake Mhe. Mama Mariam ametoa wito kwa Uongozi na
Wafanyakazi wa Benki hiyo kuendelea kufanyakazi vizuri zaidi kama
viashiria vinavyoonesha ufanisi mkubwa mbele yao ili waweze kufungua
fursa zaidi kwa wawekezaji kuwekeza katika sekta ya uchumi na fedha kwa
maslahi ya pande zote mbili.
Wakati huo huo Mhe. Mama Mariam Mwinyi amefanya Ziara kutembelea Ofisi ya Mke wa Rais wa Burundi na Mwenyekiti wa Taasisi inayoshugulikia Maendeleo Nchini Burundi; Mama Angeline Ndaishimiye iliopo Bujumbura, Alishiriki zoezi la upandaji mti kuashiria umoja na mashirikiano yao wakiwa viongozi wanawake ndani ya Nchi za Bara la Africa.
Katika zoezi hilo alishiriki pia Muwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya wanawake UN WOMEN kikanda - Afrika Ms. Awa Ndiaye Seck.
IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment