Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga amewasili Mkoani Tanga kwa ziara ya siku sita ya kuimarisha Chama kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024.
Alipowasili Uwanja wa Ndege wa Tanga Mhe. Hemed amepokewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Rajab Abdulrahman Abdallah, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe . Waziri Kinda Kindamba pamoja na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali na wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.
Mara baada ya mapokezi hayo Mhe. Hemed alifika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga kupokea taarifa za maendeleo ya Chama Mkoani hapo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025 ambapo amewataka wanachama na Viongozi wa CCM kuunga Mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaendelea kuwatumikia watanzania kwa miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kusimamia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Mhe. Hemed ambae ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga amewasisitiza Viongozi wa CCM Mkoa huo kuzidisha umoja na mshikamano baina yao ili kufikia dhamira ya CCM kushinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Ndg. Rajab Abdulrahman Abdallah ameeleza kuwa Mkoa wa Tanga unaendelea kunufaika na Miradi mbali mbali ya maendeleo chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo mashirikiano baina ya Viongozi Chama na wa Serikali yanasaidia kurahisisha utekelezaji wa miradi hiyo.
Ameeleza kuwa CCM Mkoa wa Tanga imeimarika kutokana na Viongozi kujishusha na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi pamoja na kueleza kuwa CCM Mkoa wa Tanga ina kila sababu ya kushinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.
Abdulrahim Khamis
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
08/10/2023
No comments:
Post a Comment