Habari za Punde

UWT Kupambano na Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja Wanawake UWT Ofisi ya Zanzibar  Tunu Juma Kondo wakati  akitoa  maelezo kuhusiana na kuanzishwa Kamati maalum ya kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji, iliopo chini ya UWT, huko Ofisi kuu ya CCM Kisiwandui Wilaya ya Mjini.

Afisa habari kutoka idara ya habari maelezo Zanzibar Takdir Ali Suweid akizungumza na  naibu wa kamati tekelezaji taifa na mjumbe wa kamati ya kupinga vitendo vya udhalilishaji  UWT Fatma Sufa kuhusiana na wanavyokabiliana na vitendo vya udhalilishaji, huko Ofisi kuu za CCM Kisiwandui Mjini Unguja.

Picha na Fauzia Mussa –Maelezo Zanzibar.

Wananchi wametakiwa kushirikiana na Kamati maalum ya kupiga vita vitendo vya Udhalilishaji, ilioanzhishwa na Umoja Wanawake Tanzania UWT ili kuweza kuviondosha vitendo hivyo katika jamii.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja Wanawake Tanzania UWT Ofisi ya Zanzibar Tunu Juma Kondo wakati wa kikao kazi cha kujadili majukumu ya Kamati hiyo, huko Ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwanduwi Wilaya ya Mjini.

Amesema vitendo vya Udhalilishaji vinaongezeka siku hadi siku hivyo amewaomba Wananchi kushirikiana na Kamati hiyo ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia malengo yaliokusudiwa ya kukomesha vitendo hivyo.

Aidha amesema Kamati hiyo itashuka moja kwa moja chini kwa Wananchi katika Vijiji, Shehia,Wadi, Majimbo, Wilaya na Mkoa, waweze kushirikiana na Waratibu wa Wanawake na Watoto waliopo katika Shehia ili kupata taarifa na kuweza kuzifanyia kazi.

Hata hivyo amesema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ipo mstari wa mbele kupinga vitendo vya udhalilishaji hivyo amewaomba Wanawake wenzake kuiunga mkono kwa kuacha muhali na kutaoa Ushahidi Mahakamani wakati wanaposhuhudia vitendo hivyo.
 
"Suala la udhdliishaji limekuwa Mtihani mkubwa tulipe kipao mbele sana tena sana kwa sababu ,vitendo vya udhilishaji vinapokea wathirika wakubwa ni Wazazi" alisema  Naibu huyo.

Kwa uapnde wake Mjumbe wa Kamati ya Uchalilishaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Fatma Sufa ameupongeza Uongozi wa UWT kwa kumteua katika Kamati hiyo na kuahidi kufanya kazi kwa ufanisi ili kuweza kufikia malengo yaliopangwa.

Amesema kamati itahakikisha inapita maeneo yote ili kutoa elimu ya udhalilishaji, ushauri na na kuwaomba Wananchi kuiunga mkono ili Wanawake na Watoto wabaki sala na kuetekleza wajibu wao wa kuenda Skuli na Mdrsa kusoma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.