Aidha, imetaja azma ya
kuzifungua barabara kubwa zenye hadhi ya juu kutoka Wete hadi Chake na kutoka
Chake hadi Mkoani mwishoni mwa mwaka huu ili kukikuza kisiwa Cha Pemba
kibiashara na uwekezaji.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyasema hayo Hotel
“the mora” alipozindua jina jipya la hoteli hiyo kutoka la zamani la “Emarald”
huko Matemwe, Mkoa wa Kasakazini Unguja.
Dk. Mwinyi
amesema tayari Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Pemba ili
ndege za kimataifa zitue kisiwani humo.
Akizungumzia
maboresho makubwa ya uwanja wa Ndege wa Kimaifa wa Abeid Aman Karume Rais Dk.
Mwinyi amesema mara baada ya kukamikila kwa hatua kubwa ya jengo namba 3 ambalo
kwasasa linafanya vizuri kimataifa, Serikali pia inafanya matengenezo makubwa
kwa “Terminal 1 & 2 na ujenzi mpya wa (terminal 4) ili kuboresha mazingira
ya uwekezaji na Utalii nchini.
Pia, Rais
Dk. Mwinyi ametaja faida za uwekezaji nchini, nakueleza kuwa umechangia
asilimia kubwa ya maendeleo ya nchi kutokana na kodi wanazolipa wawekezaji kwa Serikali
ambazo hutumiwa kuboresha huduma za jamii ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya
barabara na mawasiliano, ujenzi wa skuli mpya, hospitali, masoko, pamoja na
kusambazwa kwa maji safi na Salama.
Rais Dk.
Mwinyi pia, alieleza jinsi uwekezaji unavyofungua fursa nyingi kwa wazawa wakiwemo
wakulima, wafugaji, wavuvi na wafanyabiashara kupata soko la uhakika la bidhaa
zao kupitia mahoteli mbalimbali yaliopo nchini.
Alisema,
Serikali huwalazimisha wawekezaji wa maeneo yote kuboresha huduma za jamii
maeneo yote yaliyopitiwa na uwekezaji ikiwemo kujenga vituo vya afya, ujenzi wa
vituo vya watoto yatima pamoja na mahitaji husika ya maeneo hayo.
Hata hivyo,
Rais Dk. Mwinyi alimwagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Uwekezaji,
Sharif Ali Sharif kuwasimamia wawekezaji wote kununua mahitaji yote
yanayozalishwa nchini kabla ya kuagiza nchi ya nchi ili kutanua fursa kwa
wajasiriamali wazawa na wafanyabiashara wa ndani.
Akizungumzia
uwekezaji wa “Hotel the mora” Rais Dk. Mwinyi amesema imeekeza zaidi ya dola za
Kimarekani milioni 600 pamoja na kutoa ajira 600 kwa wazawa na wenyeji nchini.
Akisifia
uzuri na haiba ya kisiwa cha Zanzibar,
Mkugenzi Mwendeshaji wa kampuni
ya “Tui Group, wamiliki wa “Hotel the mora” Sebastian
Abel amesema Zanzibar ni kisiwa chenye hadithi nyingi nzuri zenye kumvutia kila
mgeni anaetembelea pia ni zawadi na sehemu salama ya uwekezaji na biashara ndio
maana wamevutiwa na kuwekeza nchini.
Naye,
Waziri Sharif aliwahakikishia ushirikiano wa hali ya juu wawekezaji wote
waliopo nchini pia amesema maendeleo makubwa kwenye sekta ya uwekezaji ni
juhudi za Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Saleh
Saad Mohamed, amesema “Hoteli the mora” yenye hadhi ya nyota tano inamilikiwa
na kampuni ya “Tui Group” ambayo tayari imewekeza nchi zaidi ya dola za
kimarekani milioni 500 kwenye sekta ya Utalii kupitia hoteli zake za ‘RIU”
iliopo Nungwi, “ TUI BLUE” ya Mangapwani na “the mora” ya Matemwe.
Alisema,
kampuni ya “Tui Group” pia inatarajia kutambulisha jina lake jengine la “
Robinson” ambalo tayari ZIPA imelipatia chei
cha uwekezaji wa mdadi mkubwa wenye thamani za dola za kimarekani
milioni 50, kupitia kampuni ya “Blackstone Limited”
Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja Rashid Hadid amsema mkoa huo una hoteli 316 kati
ya hizo 18 zina hadhi ya nyota tano kwa ujumla wake zinachangia asilimia 61 za
pato la taifa kutoka kwenye sekta ya Utalii mkoani humo, aidha ameeleza juu ya
mkoa wao unavyotumia utalii wa fukwe kukuza sekta hiyo kupitia Sera ya Uchumi
wa Buluu.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment