Na.Mwanajuma Juma.
TIMU ya soka ya Alqaida imeungana na timu za Meli Nne City na Mboriborini kuyaaga mashindano ya Yamle Yamle Cp 2024, baada ya kufungwa na Ponchiki bao 1.0 katika mchezo wa robo fainali ya tatu uliochezwa juzi Mao Zedong.
Katika mchezo huo ambao ulichezwa majira ya saa 10:00 za jioni ulionesha ushindani wa hali ya juu hasa katika kipindi cha pili.
Miamba hiyo iliyocheza kwa kila mmoja kuusoma mchezo wa mwenzio na kumaliza dakika 45 za awali wakiwa hawajafungana.
Kipindi cha pili kilianza na miamba hiyo kuendelea kushambuliana kwa zamu na kufika dakika ya 59 Ponchiki ikajipatia bao lake hilo la pekee lililofungwa na Mohammed Ali.
Mpaka sasa wakati timu tatu zikiyaaga mashindano hayo, timu tatu nyengine zimesonga mbele katika hatua ya nusu fainali.
Timu hizo ni Miembeni SC iliyoifunga Meli nne City kwa penalti 4-3, JKU Academy iliyoifunga Mboriborini mabao 3-0 na Ponchiki ambayo iliifunga Alqaida bao 1-0.
No comments:
Post a Comment