Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo
na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi Duniani (GCA)
Prof. Patrick Verkooijen. Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa
29 wa Nchi Wanachama
wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29)
unaofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya Tanzania na Taasisi hiyo katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mazungumzo hayo
yamehudhuriwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Cosato Chumi, Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Cyprian Luhemeja, Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa (New York) Mhe. Balozi Hussein katanga
pamoja na Mshauri wa Rais kuhusu mabadiliko ya tabianchi Dkt. Richard Muyungi.
No comments:
Post a Comment