Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Mwinyi baada ya sala ya Ijumaa aliendeleza utaratibu wake wa kuwatembelea Wananchi na kuwajulia hali Wagonjwa katika maeneo mbalimbali.
Aliowatembelea leo ni aliekuwa Mbunge na Naibu Waziri Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mshauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Awamu ya Saba, Dk. Maua Abeid Daftari anaeishi Beit Ras Wilaya ya Magharibi A.
Msanii Mkongwe wa sanaa za Filamu na Maigizo Zanzibar Bibi Mwanamwema Khamis Juma, maarufu Bi Njiwa.
Mwengine ni Bi. Halima Muhamed, Mjane wa aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama, Marehemu Borafya Silima wanaoishi Mwera Mtofaani.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment