Ujumbe wa Timu ya kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Wataalam kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Wakiambatana na wataalam Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar wakielekezwa jambo sehemu ambapo ujenzi wa Bandari na kiwanda cha kuchakata samaki kinapojengwa.
Ujumbe wa Timu ya kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Wataalam kutoka Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Wakiambatana na wataalam Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TAMISEMI, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar wakielekea sehemu ambapo ujenzi wa Bandari na kiwanda cha kuchakata samaki kinapojengwa.
Wakiwa katika eneo la Bandari ya Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Timu hiyo imetembelea na kuona eneo ambalo kiwanda cha kuchakata na kutunza samaki, kinajengwa ikiwa ni pamoja na chumba cha uzalishaji wa barafu yaani "ice plant".
Pamoja na hayo timu hiyo imepata fursa ya kutembelea eneo la Kilwa Kivinje Mkoani Lindi, ili kuona eneo ambapo "AFDP" Kupitia ufadhili wa "IFAD" inajenga eneo litakalotumika kwa kuanika dagaa na kuchakata samaki, mara baada ya kuwavua.
Mradi huo unajengwa ili kuwasaidia wavuvi na wachuuzi wa samaki hasa akina mama, ambao wamekuwa ni mstari wa mbele katika kufanya bishara ya samaki na dagaa.
Kukamilika kwa mradi utakuwa ni ukombozi kwa wafanyabiashara, ambao walikuwa wakipata taabu eneo la kuanika dagaa hasa wakati wa masika.
No comments:
Post a Comment