Habari za Punde

Wakili Mkuu wa Serikali Akutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jijini Arusha


Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) akizungumza na Rais wa Mahakama wa Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Dkt. Possi ya kujitambulisha na kuona namna Mahakama hiyo inavyofanya kazi jijini Arusha.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akimkabidhi Jarida la Wakili Mkuu Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud alipotembelea Mahakama hiyo kwa lengo la Kujitambulisha na kuona namna Mahakama hiyo inavyotekeleza majukumu yake Jijini Arusha.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally possi akipokea zawadi ya Taarifa za Kesi kutoka kwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud alipotembelea Mahakama hiyo kwa lengo la kujitambulisha na kujionea namna Mahakama hiyo inavyotekeleza majukumu yake jijini Arusha. 

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt Ally Possi (wa nne kushoto) na ujumbe wake akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud (wa nne kulia) baada ya kutembelea Mahakama hiyo kwa lengo la kujitambulisha na kujionea namna Mahakama hiyo inavyotekeleza majukumu yake jijini Arusha.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.