Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi (katikati) akiongea na watumishi wa Ardhi Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dodoma pamoja na jiji la Dodoma Novemba 8, 2024 ambapo ametoa siku 30 kwa kwa watumishi hao kutatua migogoro ya ardhi katika jiji la Dodoma na kupata majawabu ifikapo Desemba 10 2024. Kushoto ni Naibu Waziri Mhe. Geophrey Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga
Baaadhi ya
watumishi wa Ardhi Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dodoma pamoja na
jiji la Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi
Mhe. Deogratius Ndejembi Novemba 8, 2024 ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini
Dodoma.
Na Eleuteri Mangi, WANMM
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa siku 30 kwa watumishi wa Ardhi jiji la Dodoma kutatua migogoro na changamoto za ardhi na kupata majawabu ifikapo Desemba 10 2024.
Waziri Ndejembi amesema hayo Novemba 8, 2024 wakati wa kikao chake na watumishi wa Ardhi Ofisi ya Kamishna wa Msaidizi Ardhi mkoa wa Dodoma pamoja na jiji la Dodoma ambapo amesema mwelekeo wake ni utendaji kazi kwa weledi, kutenda kazi kwa haki na kuwahudumia wananchi kwanza.
Waziri Ndejembi amesema watumishi hao kama watashindwa kutatua changamoto ya ardhi katika jiji hilo atawachukulia hatua kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kupanga jiji la Dodoma vizuri kwa nafasi kwa kutenga maeneo ya bustani za kupumzikia na maeneo ya michezo ya watoto kwa kuangalia mahitaji ya sasa na baadaye.
Aidha, amewaagiza watumishi wa serikali ambao ni wa ajira ya kudumu wafanye kazi ya kuingia kwenye mfumo na kutoa huduma kwa wananchi na kusisitiza kazi hiyo isifanywe wa watumishi wa mkataba na wanaojitolea ili kumaliza changamoto ya kupanga kiwanja kimoja kwa watu wawili kwa wakati mmoja.
Waziri Ndejembi amewataka watumishi ambao hawawezi kuendana na kasi ya Wizara na ukuaji wa MakaoMakuu katika jiji la Dodoma waseme ili wahamishiwe sehemu nyengine na kuongeza kuwa asilimia 90 ya watumishi wa jiji la Dodoma hawapokei simu za wanamchi wanaouliza na kuhitaji huduma za ardhi kuhusumaeneo yao na kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu.
Amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga kuwasiliana na vyombo vya dola kuwachukulia hatua watumishi wawili Herman Chizoza na Palangyo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi kwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni sita kwa wateja waliokuwa wanahitaji huduma ya Ardhi katika ofisi hizo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendekeo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewata Wakurugengenzi wote kusimamia maagizo ya viogozi na kuwasisitiza watumishi hao kuyajua wayatekelezamaagizo yote yanayotoka kwenye mfumo ili sekta ya ardhi itoe huduma stahiki kwa wananchi na kusemwa vizuri.
Naye Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga amesema wameyapokea na watayafanyia kazi maelekezo ya Waziri Ndejembi na kuwasisitiza kupokea simu za wananchi kwa kuwa hao ndiyo waajiri wao, wasipopokea simu wananchi waende wapikwa kwa watumishi hao ndiyo wenye majawabu ya mahitaji ya wananchi.
No comments:
Post a Comment