Habari za Punde

Waziri Tabia atoa Sadaka Kwa Waumini wa Dini ya kikiristo

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita akizungumza na Waumini wa Dini ya Kikiristo mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula Mbali Mbali na fedha taslim katika Kanisa la Parokia ya MT  Mikaeli Malaika Mkuu, Mpendae. Wilaya ya Mjini.

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita ametoa Sadaka ya Vyakula mbali mbali na pesa Taslim  kwa waumini ya Dini ya Kikiristo ili kuwasaidia katika Skukuu ya Pasaka .

Akitoa Sadaka hiyo  Katika Kanisa la 
Parokia ya MT  Mikaeli Malaika Mkuu , Mpendae, Wilaya ya Mjini  amesema Serikali inawathamini na  kuwapenda waumini wa Dini zote hivyo ni vyema kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum ikiwemo watoto yatima na wajane ili waweze kufurahia sikukuu 

Aidha amesema ipo haja ya Mashirika na Watu  wenye uwezo kuwasaidia waumini hao  kutokana kuwa  wengine wanaishi Katika mazingita magumu jambo ambalo litawasaidia kujikwamua kimaisha 

Waziri Tabia alisema ataendelea  kushirikiana  na waumini hao  kwa kuwapatia  misaada mbalimbali ili waweze kuendesha shughuli zao.
Baadhi ya Masister na Waumini mbali mbali wa Dini ya Kikiristo wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita (hayupo pichani) katika Kanisa la Parokia ya MT  Mikaeli Malaika Mkuu, Mpendae. Wilaya ya Mjini.



Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita (wa pili kushoto) akikabidhi fedha taslim kwa Paroko Padre Antony Kantu (wa kwanza kushoto)  na Waumini wa Dini ya kikiristo katika Kanisa la Parokia ya MT  Mikaeli Malaika Mkuu, Mpendae. Wilaya ya Mjini.
Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Mjini Asteria Moris  Ambros akitoa shukrani kwa Viongozi Wakuu kwa kuonesha mashirikiano yao huko katika Kanisa la Parokia ya MT  Mikaeli Malaika Mkuu, Mpendae. Wilaya ya Mjini.
 Baadhi ya Masister na Waumini mbali mbali wa Dini ya Kikiristo wakimsikiliza Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita (hayupo pichani) katika Kanisa la Parokia ya MT  Mikaeli Malaika Mkuu, Mpendae. Wilaya ya Mjini.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Amani Kichama  Fransisca  Camilius Clement akitoa neno la shukrani kwa  Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita katika Kanisa la Parokia ya MT  Mikaeli Malaika Mkuu, Mpendae. Wilaya ya Mjini.

Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Amani Kichama  Fransisca  Camilius Clement amesema kushirikiana  pamoja na Waziri Tabia Katika kusherehekea Pasaka imeonyesha dhahiri kwamba Viongozi wa Serikali kuwajali waumini hao.

Amesema anaamini kwamba Serikali haina Dini,Ukanda Wala ukabila hivyo ni vyema kuwasaidia watu wa makundi Mbali Mbali ya mahitaji ikiwemo watoto yatima na wajane .

Kwa Upande wa Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Mjini Asteria Moris  Ambros amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Hussein Mwinyi kupitia  Waziri Tabia Kwa kutoa Sikukuu katika Kanisa la Mtakatifu Mikaeli ili kusherehekea vizuri Pasaka .

Akizungumza Kwa niaba ya Wajane na watu wenye mahitaji Maalum Mkuu wa Kanisa,Paroko Padre Antony Kantu amesema wamefarijika Kwa msaada huo na kuwaombea wazidishe juhudi kuendeleza kuwasaidia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.