Na Haji Nassor ZJMMC.
WANAJAMII wanaoishi katika maeneo yenye michirizi inayopitishia maji ya mvua wametakiwa kuanza kuisafisha kabla ya mvua za masika hazijashamiri, ikiwa ni maandalizi ya kujikinga na mardhi mbali mbali ya mripuko wakati mvua zitakapoanza kunyesha.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na mtaalamu wa Mazingira kutoka Idara ya Mazingira Zanzibar, Hamza Zubeir Rijali ofisini kwake Maruhubi mjini Zanzibar, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kuhusu majukumu ya jamii katika kipindi hiki.
Alisema ardhi ya Zanzibar yenye maumbile ya mabonde, vilima na tambarare inaipa nafasi jamii kuzingatia hali kama hiyo na kufanya kila liwezekanalo katika kusafusha michirizi ili maji yasikwame pale mvua zitakaposhamiri.
Mtaalamu huyo alisema pamoja na kuwepo taasisi mahususi inayosimamia usafi lakini suala la kujilinda nalo ni muhimu kwa sababu chochote kitakachotokea hakitamchagua mtu,
''Ni kweli kwamba ipo taasisi yenye Mamlaka ya kuisafisha mitaro, michirizi na mji kwa ujumla lakini wakati tunapokuwa tunainga katika kipindi kama hichi kazi hiyo huwa haina mwenyewe kila mmoja anawajibika'', alifafanua.
Aidha, Hamza amekemea tabia ya baadhi wananchi ,wanaoishi karibu na mitaro hiyo kuifanya kama sehemu ya jaa jambo linalowzesha kuzuka mafuriko.
Alisema anashangazwa na baadhi ya watu wanaoishi karibu na michirizi hasa iliokwisha jengwa kwa ajili ya kurahisishia maji kupita kwa kasi lakini baadhi ya wakati wamaeneo kama hayo wameigeuza michiri kama sehemu ya kutupia taka za majumbani.
Ni kawaida katika baadhi wa maeneo ya mji wa Zanzibar wakati mvua zinaponyesha kutokezea mafuriko ambayo husababishwa na mitaro kuziba kwa kujaa taka taka zinazotupwa na wananchi wenyewe.
No comments:
Post a Comment