Habari za Punde

FAHAMU MAAFA YANAYOIKUMBA LUGHA YA KISWAHILI (1)

Na Haji Suleiman Amour
TAABU za kipindi ambazo kikisha kile kipindi tabu huondoka.Mfano tabu ya baridi , kikisha kipindi cha kipupwe, tabu ya baridio huondoka yenyewe.

Hali kadhalika, Kiswahili kilianza kwa tabu nyingi za maafa.Kuna kipindi hutokea wataalamu wakakizulia Kiswahili tabu Fulani, ikapokewa na watu wasiokuwa na elimu ya fahamu wala elimu ya kalamu, ikawa tabu kwa Kiswahili, hakina raha.

Kwani yale maafa huwa yanaifisidi ile lugha ya Kiswahili. Wakati mmoja unakumbukwa ile sintaksi ya Kiswahili iliponyang’anywa sheria yake ya viambishi ngeli. Viambishi ambavyo vinapatikana awali ya kitenzi au sifa, wengine wanaita vivumishi.

Maneno ‘tosha’ na ‘husu’ yalitiwa katika idhilali ya kunyang’anywa viambishi vyao kwenye nafsi ya tatu.

Vitabu vingi vipo vimeandikwa ‘sababu tosha’, sehemu husika’. Mtindo huo au matumizi hayo ya lugha yanafiosidi lugha.

Ufisadi uko wapi?

Uko pale unapotumika ikawa vigumu kueleweka iwapo sentensi au maelezo yale ni umoja au wingi. Sehemu husika ni sehemu moja au sehemu nyingi, hospitali husika ni hospitali moja au nyingi. Sababu tosha- ni sababu moja au nyingi.

Maafa ya pili ya ngeli ni mtindo wa kulitoa jina lililopangwa na wasemaji wa lugha katika ngeli fulani, likatiwa katika ngeli nyengine wanayoichagua wale watu ambao hawana elimu ya kalamu wala elimu ya fahamu.

Wasio na elimu ya kalamu ni wale watu ambao hawakusomeshwa na mtu yeyote isipokuwa wanasikia matamko na kuyafuata bila ya kuyafahamu misingi yake.

Kumuita maiti, maiti hii na mtangazaji wa redio na televisheni ya Unguja naye akadakia ‘maiti imeokotwa’, maiti imepewa wenyewe, maiti imeharibika.

Muongo huyu ambaye alizaliwa Tumbatu, Pemba, Unguja maisha yote hakuwahi kupata kusikia maiti kuingizwa katika ngeli ya imezikwa, zimezikwa na yako makabila mtu anaitwa ‘mitu’. Mtu huyu kwao ‘mitu
hii’. Kwa watu hawa na maiti hii kamwe hawi maiti hii.

Au ndugu zetu skuli wanaziita ‘shule’. He! Ni wengi hawa. Nao njia yao ni ile ile ya kuiga. Amewasikia watu walioogopa kuita skuli-sukuli au sukli wakaona afadhali watumie neon la Ulaya la Wajerumani. Shule- neno ambalo halina ‘s’ isiyo irabu.

Hii ndiyo sababu idadi kubwa ya watu wasio na mazoea ya kutamka ‘s’ wanatumia neno shule. Hata wale wanaodiriki kufika skuli na kumudu kuitamka skuli wanaona si insafu kuwatupa mkono wenzao.

Ndiyo maana sisi wengi hatudahili sana jambo la skuli kuitwa shule- kwa Tanzania bara.

Hoja ipo hapa, wewe ulizaliwa ‘P’, vyuo vya Kurani viko unatanka ‘s’ bila ya mashaka iko haja gani kuandika nemesoma shule ya Michakaeni, unawaunga mkono akina nani?

Yako maafa ya Kiswahili yanazushwa na watu wenye nafsi hafifu.Nafsi hizi huwa ziko tayari zifiche hata kwao kusijulikane zinapotia shaka kuna kule kwao kunadharauliwa au wao wataonekana watu duni, kwa kujulikana kuwa ni watu wa kule.

Hawa ni wale wanaoogopa wasitambulikane kuwa kwao ni shamba. Siku hizi ni rahisi kujitoa kwenye ushamba, ukajitia kwenye umji, baada ya kuja kimji kipya.

Kimji kipya ni ki-Dar es salaam au ki-Bara. Ukishasema ki-Dar es salaam na ukatamka ki-Bara, simshamba tena!

Walimu wa skuli za serikali kuanzia wale wa darasa la kwanza mpaka wale wa kidato cha sita. Ukisema wanasomesha unasema ki-shamba, ila useme wanafundisha.

Anayesomesha Histori, anafundisha Historia, anayesomesha Kemistri kwa kimji kipya ofisa wa kilimo umwite bwana shamba/bibi shamba.

Utadhani ofisa u mtaalamu wa kilimo serikali inamuajiri kwa ubwana shamba wake au ubibi wake.

Serikali inayemtaka ni msomi wa kilimo na jina lile la bibi shamba/ bwana shamba linasahaulisha serikali kuzingatia promosheni ya ofisa, badala yake inakua bibi-lini bibi anafikiriwa kutoka daraja moja ende jengine.

Maradhi hayo yameletwa na kimji kipya, kondwe kuitwa ‘shamba’.Shamba ni ardhi ya tajiri, kimji kipya konde zinaitwa mashamba.

Uigaji umekithiri. Uigaji una madakiaji na wapokeaji. Uigaji na udakiaji kunafisidi lugha. Usikubali lugha ya uigaji hata ikatumbukizwa katika hotuba uliyoandikiwa uisome waka katika mazingira uyatumie.

Maafa mengi huwa yana madhara kwa yanayowafika. Tuchukue maafa ya maana za maneno ya Kiswahili kuwa hazimo katika makamusi ya Kiswahili ndipo unapata wasemaji wengi wa lahaja ya mashariki ya Kiswahili wanakuwa rahisi wa upokeaji wa udakiaji.

Wao ni wakulima, lakini ardhi zinazolimwa hazikuanishwa zote. Hapo konde wakiambiwa shamba, nao konde ya maweni wanaita shamba – mashamba ya kilimo cha maweni.

Shamba gani linaanza kwa chenge. Je, iwapo watu ishirini au zaidi watalima ushirika wa mtama kwa chenge , lile ni shamba au konde- neno gunda hulipati katika kamusi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.