Habari za Punde

VIONGOZI WA DINI WAOMBA MVUA KULINUSURU MTERA

Na Nalengo Daniel, Dodoma

KUFUTIA kupungua kwa kina cha maji katika bwawa na Mtera, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, wamefanya ibada maalumu, kuombea mvua inyeshe ili kunusuru matatizo ya ukame na mgawo wa umeme unaondelea nchini.


Akizungumza wakati wa ibada maalumu ya kuombea mvua, iliyojumuisha madhehebu mbalimbali ya dini, Askofu mkuu wa kanisa la Good news for all Charles Gadi, alisema viongozi wa madhehebu ya dini hawatavumilia wananchi, kuendela kuingia kwenye matatizo ya ukame na mgawo wa umeme, na kwamba wanaamini kupitia maombi Mungu anaweza kulinusuru taifa na ukame huo.

Askofu Gadi alisema Tanzania imejaliwa kuwa na mito mingi, vyanzo vingi vya maji, na hakuna sababau ya kuwa na janga la njaa na ukame, lakini kutokana na watu wake kuendela kumkose Mungu, yametokea mabadiliko ya kukosa mvua, na kusababisha ukame na kwamba bila kufanya maombi, itakuwa vigumu kuondokana na majanga ya ukame, yanayochangia ukosefu wa chakula.

Alisema machafu yamezidi na kuyataja baadhi kuwa ni ,kumuasi mungu, umwagaji wa damu zisizokuwa na hatia, utoaji wa mimba zisizokuwa na hatia, ulawiti na rushwa, na kwamba ili kulinusuru taifa na janga hili, wananchi wanatakiwa kufanye toba na kumrudia mungu.

Askofu Gadi alisema ataongoza toba, kwa niaba ya watanzania ya kuwaunganisha na mungu, na kwamba ana imani kuwa Mungu ni mwema, na atafanya kwa kile wanachokiomba kwani si, kusudio lake kuona wanadamu wanateseka kwa njaa, ukame na giza.

Alisema kwa njia ya maombi na kufanya toba, Mungu atatenda miujiza na hakuna sababu ya kusubiri hadi wakati wa mvua za masika, wakati wananchi wakiendela kuumia na kuathirika na matatizo mengi yanayosabaishwa na ukame.

kabla ya maombi kufanyika,Kaimu Meneja kitendo cha uzalishaji umeme Mtera, Steven Mpfumbutsa alisema upungufu wa maji katika bwawa hilo kwa sasa ni mita za ujazo 690.4 na endapo zitafikia 620.00 italazimika kusimamisha shughuli za uzalishaji umeme katika bwawa hilo

Mpfubutsa alizitaja athari wanazozipata, kufuatia kupungua kwa maji katika bwawa hilo, kuwa ni kuathiri shughuli za uzalishi umeme , kupungua kwa kipato kwa wakazi wa mikoa ya Iringa na Dodoma, wanaoishi kando kando ya bwawa hilo na kuendesha maisha yao kwa kutegemea shughuli za uvuvi.

Athari nyingine, ni ukame ambapo baadhi ya wananchi wanalazimika kuishi maisha ya kuhamahama, hasa wafugaji ambao wanategema maji katika bwawa hilo, kwenye majosho ya mifugo pamoja na wakulima waliokuwa wakitegema kilimo cha mvua na umwagiliaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.